LAYIII
‘Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaokaribiana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mfano; Mfumuko wa Bei wa mwezi Agosti, 2015 nchini Kenya umefikia asilimia 5.84 kutoka asilimia 6.62 mwezi Julai, 2015 na Uganda umefikia asilimia 4.80 kutoka asilimia 5.4 mwezi Julai, 2015′ – Ephraimu Kwesigabo
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu
za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo aliitisha
mkutano wa vyombo vya habari leo Sept 8 kutoa taarifa ya takwimu ya
mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Agosti, 2015.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo alisema..’Mfumuko
wa bei wa taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la
kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya
binafsi.Mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti, 2015 umebaki kuwa asilimia 6.4
kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji
wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioshia mwezi Agosti, 2015
imekuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioshia mwezi Julai, 2015′ – Ephraimu Kwesigabo
‘Mfumuko
wa bei wa mwezi Agosti, 2015 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka
kwa asilimia 0.02 ikilinganishwa na asilimia 0.41 ilivyokuwa mwezi
Julai, 2015. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 158.81 mwezi Agosti, 2015
kutoka 158.78 .mwezi Julai, 2015. Kuongezeka kwa fahirisi za bei
kumechangia hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za
vyakula.Baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia
kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na gesi kwa asilimia 2.0 mafuta ya taa
kwa asilimia 2.3, mazulia kwa asilimia 1.4, dizeli kwa asilimia 3.8 na
petrol kwa asilimia 8.3′ – Ephraimu Kwesigabo
‘Thamani ya shilingi ya Tanzania mwezi
Agosti, 2015 ikilinganishwa na mwezi septemba 2015 uwezo wa shilingi 100
ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 62 na
senti 97 mwezi Agosti, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 ikilinganishwa
na shilingi 62 na senti 98 ilivyokuwa mwezi Julai, 2015‘ – Ephraimu Kwesigabo‘Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaokaribiana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mfano; Mfumuko wa Bei wa mwezi Agosti, 2015 nchini Kenya umefikia asilimia 5.84 kutoka asilimia 6.62 mwezi Julai, 2015 na Uganda umefikia asilimia 4.80 kutoka asilimia 5.4 mwezi Julai, 2015′ – Ephraimu Kwesigabo
No comments:
Post a Comment