LAYIII
Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambaye
amekuwa akiwakwaza mashabiki wa klabu hiyo kwa tabia yake ya kutopenda
kutoa fedha nyingi ili apate mchezaji wa kiwango cha juu, Wenger ni kocha ambaye amekuwa na misimamo ya kutopenda kununua wachezaji kwa gharama ya juu.
Hii ni taarifa kutoka kwake kwani baada
kutokubali kukiri wazi kuwa ana mpango wa kufanya usajili msimu huu,
August 27 imebidi aweke wazi kama sehemu ya kuwatuliza jazba mashabiki
wa timu ambao walikuwa wakiamini kuwa huenda kocha huyo hana mpango wa
kusajili tena msimu huu.
“Nipo bize
masaa 24 kwa siku nina team inayonizunguuka inafanya kazi usiku na
mchana kutafuta ufumbuzi wa suala hili lakini bado hatuko karibu
kumsajili mchezaji yoyote. Wapo maalum ambao umewalenga wanaweza
kupatikana kwa sababu ya vitu fulani lakini najiamini hadi dakika ya
mwisho tutakuwa tumepata ufumbuzi” >>> Wenger
Hadi hivi sasa Arsene Wenger amefanya usajili wa golikipa Peter Cech kutokea katika klabu ya Chelsea hivyo mashabiki wa Arsenal wanamashaka kwani bado wiki moja dirisha la usajili lifungwe.
No comments:
Post a Comment