LAYIII
Wema Sepetu alikuwa ni miongoni mwa watu
wanaogombea ubunge viti maalumu mkoani Singida lakini hakuwa na bahati
ya kushinda au kuingia bungeni kutokana na kura zake kuwa ndogo.
Staa huyo aliibuka na kupata kura za
maoni za ubunge 90 huku wagombea wenza wakiongoza kwa
kura za maoni,
Aysharose Mattembe (311), Martha Mlata ( 235) na Diana Chilolo (182).
Japokuwa hakushinda katika
kinyang’anyiro hicho Leo July 26 alipata mapokezi makubwa kutoka kwa
mashabiki wake, nimekusogezea hizi picha hapa za mapokezi.
No comments:
Post a Comment