Usajili wa kipa Mhispania David De Gea kuelekea klabu ya Real Madrid kwa sasa inaonekana kama huenda usitokee tena hivi karibuni baada ya klabu hii ya Hispania na wenzao wa Manchester United kushindwa kufikia makubaliano .
Manchester United imegoma kabisa kufanya mazungumzo na Real kuhusiana na De Gea kutokana na Wahispania hao kushindwa kutimiza masharti ambayo United imeyaweka katika mazungumzo hayo .
United imewaambia Real kuwa endapo wanamtaka De Gea basi wakubali kumruhusu beki Mkongwe Sergio Ramos ajiunge na United au Gareth Bale jambo ambalo vijana hawa wa Florentino Perez amelikataa katakata.
Tayari Real Madrid imesajili kipa Kiko Castilla ambaye amejiunga tokea Real Sociedad huku Keylor Navas akichukua mikoba ya kipa namba moja baada ya gwiji Iker Casillas kuondoka ambapo amejiunga na Fc Porto .
Real Madrid kwa muda mrefu wamekuwa wakimtaka David De Gea ambaye wamepanga kumfanya mrithi rasmi wa Iker Casillas huku United ikigoma kabisa kuzungumza dili yoyote inayomhusu De Gea.
Vyanzo vingine vya habari vimesema kuwa Real Madrid inajiandaa kusubiri mpaka mwishoni mwa msimu huu mpya wakati ambapo mkataba wa De Gea utakapokuwa unamalizika na kumfanya kipa huyu kuwa mchezaji huru hali itakayowafanya Real wamsajili bure .
No comments:
Post a Comment