LAYIII
Safari ya kuelekea Kombe la Dunia 2018 Urusi imeshaanza kwa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA
kupanga makundi na ratiba ya michuano hiyo ili kupata timu
zitakazoshiriki fainali hiyo June 2018 Urusi… Droo ya kupanga makundi
imefanyika July 25 St Petersburg Urusi.
Kufuatia kupangwa kwa makundi hayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itaanza kucheza hatua ya mtoano na timu ya taifa ya Malawi October 5 2015 kabla ya
kucheza mechi ya marudiano October 13 2015.
Endapo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itapita kwa kuifunga Malawi , itakutana na timu ya taifa ya Algeria na mshindi kati yao ataingia hatua ya makundi.
Hata hivyo Taifa Stars ambayo inanolewa na Charles Mkwasa chini ya msaidizi wake Hemed Morocco bado ina mechi ya kuwania kufuzu kucheza AFCON 2017 Gabon na timu ya taifa ya Nigeria September 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment