LAYIII
Bingwa Floyd Mayweather kaingia kwenye headlines nyingine, kila mtu anajua kwamba Floyd ndio anayeongoza kwa kulipwa vizuri kwenye list ya Wanamichezo duniani, ni kweli kashindwa kulipa dola 200,000?
Floyd Mayweather amenyang’anywa mkanda wake aliomshinda Manny Pacquiao?
Hilo ndio deni lake ambalo ilitakiwa alipie ada yake kwenye Shirikisho la Ngumi Duniani WBO, mwisho wa siku ambayo jamaa ilitakiwa afanye malipo hayo ilikuwa July 03 2015…
Mpaka sasa hivi jamaa hajafanya malipo hayo na yamefanyika maamuzi
magumu kumnyang’anya mkanda wake alioshinda baada ya kumpiga Emmanuel Manny Pacquiao.
Iwapo Mayweather akinyang’anywa mkanda, Timothy Bradley atakuwa ndio Bondia anayeushikilia mkanda huo… Deni lake ni kama Milioni 444 kwa Tshs, sio kiasi cha pesa ambacho Floyd hana uwezo wa kulipia kabisa !!
Floyd Mayweather
baada ya ushindi wake wa May 2 2015 aliwahi kusema kwamba ataachia
mikanda yake yote ili mabondia wachanga wapate nafasi ya kuishindania
pia.
Mayweather
ambae bado anaishikilia mikanda ya ubingwa wa uzito wa kati bado anayo
nafasi ya kukata rufaa kujiokoa kwenye kitanzi cha uamuzi huo kabla
ya July 20 2015.
No comments:
Post a Comment