LAYIII
Utapenda kuona matembezi aliofanya VeeMoney Johannesburg South Africa. (Pichaz)
Vanessa Mdee (Vee Money) ni msanii wa Bongo Fleva anaeipeperusha bendera ya Tz vizuri kwenye nchi mbalimbali za Kiafrika. Akiwa anatamba na single yake mpya ya Nobody But Me VeeMoney ni miongoni mwa wasanii wakubwa sasa hivi Tanzania.
Licha ya kuwa mwanamziki Vanessa bado ni mtangazaji wa MTV ya South Africa kituo kikubwa cha burudani Africa na siku chache zilizopita alionekana kwenye kipindi cha Star Gist kinacho onyeshwa Africa Magic channel 151 kwenye DSTV.
Kwenye kipindi hiki VeeMoney anaungana na mtangazaji Vimbai Mutinhiri na pamoja wanafanya matembezi mbalimbali Johannesburg wakianzia Rand Airport Johannesburg na kutalii sehemu nyingine nyingi ikiwemo kutembelea Apartheid Museum.
Kama ulikikosa kipindi hiki unaweza kukitazama kupitia www.missvimbai.com, na hapa chini nimekuwekea picha zikionyesha jinsi matembezi hayo yalivyokuwa.
No comments:
Post a Comment