LAYIII ON SPOT
Dkt. Kitila Mkumbo akipokea tuzo ya mwanasiasa anayependwa sana na mwenye mvuto kwa jamii ambayo tuzo ilienda kwa Zitto Kabwe.
Mlezi Dkt. David Rweikiza akitoa
tuzo kwa mwanamitindo anayependwa ambayo tuzo ilienda kwa Sheria Ngowi,
alipokelewa na mwakilishi wake.
Mkurungezi wa Masoko wa Vodacom
Tanzania, Kelvin Twissa, akitoa tuzo kwa mtangazaji anayependwa ambayo
tuzo ilienda kwa Millard, tuzo ilipokelewa na mwakilishi wake
anayefahamika kwa jina la Askofu.
Mkurungezi
wa AEG LTD, Iman Kajula akitoa tuzo kwa Diamond Platinumz kama msanii
anayependwa, tuzo ilipokelewa na mwakilishi wake Nikki wa Pili.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi
wanaosoma Kitivo cha Masoko cha Chuo Kikuu UDSM (DUMA), Dkt. Ulimwengu
akitoa historia fupi ya Tuzo za ACHIVERS AWARDS katika kongamano la
wanafunzi wanaosoma Kitivo cha Masoko na Biashara lililofanyika Jumamosi
iliyopita UDSM na kukutanisha wanataaluma wengi na wajasiriamali
waliofanikiwa. Kongamano hili lilikutanisha vyuo mbalimbali ikiwemo
UDSM, IFM, CBE, na TIA.
Mkurunezi wa IPP Media, Dk.
Regnald Mengi akitoa hamasa ya wanafunzi kuweza kutumia fursa kuweza
kutengeneza mawazo ya kibiashara katika kongamano la wanafunzi wanaosoma
masomo ya Masoko na Biashara
Wanafunzi wakifuatilia kwa makini kongamano hilo la 'Marketing Forum'.
Washiriki wa kongamano
wakionekana kushangilia baada ya Dk. Mengi kuwa anatarajia kuzindua
kitabu chake kipya mwishoni mwa mwaka huu.
Mkurungezi
na Mwanzilishi wa Mwanaharakati Mzalendo Media pia Mkurungezi Mtendaji
wa Kajo Itech ambao walikuwa ni wadhamini rasmi wa kongamano hilo,
Krantz Mwantepele akiongea na wanafunzi jinsi gani wanaweza kufungua
fursa za baishara na kuweza kujiajiri kutumia mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment