NA LAYIII ON SPOT
Story za watu weusi kuuawa Marekani iligusa wengi, mmoja ya waliouawa ni kijana Freddie Gray ambaye aliuawa mikononi mwa Polisi kwenye mji wa Baltimore, Marekani.. leo iko hii nyngine inayohusu kisa cha mwanamke kunyanyaswa.
Hii
imetokea Texas Marekani, inahusu Polisi mmoja ambaye amesimishwa kazi
baada ya video moja kuwekwa kwenye mitandao ikimuonyesha kuwa kwenye
mabishano hivi na kundi la vijana wengi ambao ni weusi.
Katika
video hiyo afisa huyo anaonekana akiwalenga vijana wawili wa kiume kwa
bunduki yake, stori ilikuwa kubwa na watu hawakupenda kitendo cha Askari
huyo kumuangusha chini na kumkamata msichana mdogo anayekadiriwa kuwa
na umri wa miaka 15.
Polisi
hao waliitwa na wenyeji wa eneo hilo ambao walionekana kama kukerwa
hivi na vijana hao ambao walikuwa kwenye swimming poo.
Polisi wamesema wanachunguza juu ya ishu
hiyo, majibu yatatolewa Upelelezi ukikamilika japo Askari huyo, Eric
Casebolt kwa sasa amesimamishwa kazi.
No comments:
Post a Comment