Harrison Ford
ni mmoja ya waigizaji ambao ni mastaa wakubwa sana duniani wa movie za
Holywood,
kutokana na kufahamika kwake tukio la ajali aliyoipata limefanya vichwa vingi vya habari kwenye vyombo vya kimataifa kumzungumzia.
Harrison
amepata ajali ya ndege ndogo aliyokuwa akiendesha baada ya injini
kupata hitilafu na ndege hiyo kuanguka katika uwanja wa gofu wa Penmar, Los Angeles Marekani.
kutokana na kufahamika kwake tukio la ajali aliyoipata limefanya vichwa vingi vya habari kwenye vyombo vya kimataifa kumzungumzia.
Mtoto wa Harrison ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba hali ya baba yake iko poa, muda wowote anaweza akaruhusiwa kutoka Hospitali kwa kuwa amepata majeraha madogo.
Actor Harrison Ford.
Askari wa kikosi cha zimamoto Patrick Butler amesema Harrison alipata ajali ya kawaida, ana majeraha madogo japo kupona kwake ni kama bahati kwa kuwa ndege hiyo haikulipuka.
Shuhuda mmoja kwenye uwanja wa gofu
amesema aliiona ndege imepoteza mwelekeo na kuyumba huku ikionekana kama
ilikuwa inageuza kurudi uwanja wa ndege wa Santa Monica ilikotokea.
Umbali sio mkubwa kutoka kwenye uwanja wa Ndege wa Santa Monica na kwenye Uwanja wa Gofu ndege hiyo ilipoanguka.
Baadhi ya movies alizowahi kufanya Harrison Ford ni pamoja na ‘Enders Game‘ ya mwaka 2013 na ‘Air Force One‘
No comments:
Post a Comment