Hatimaye ile kesi ya kudaiwa kuuchafua uongozi wa
Clouds Media Group na mkurugenzi wake wa vipindi na uzalishaji, Ruge
Mutahaba iliyokuwa ikimkabili staa
wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ imetolewa hukumu ambapo mwanamuziki huyo ameamriwa kutozungumza chochote (amefungwa mdomo) juu ya walalamikaji hao.
.
wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ imetolewa hukumu ambapo mwanamuziki huyo ameamriwa kutozungumza chochote (amefungwa mdomo) juu ya walalamikaji hao.
.
Habari za kuaminika kutoka kwenye chanzo
makini zilidai kwamba hukumu ya kesi hiyo juu ya malumbano yaliyokuwa
makali kati ya pande hizo, ilikamilika hivi karibuni ambapo Jide au Lady
Jaydee alipewa maelekezo hayo.
Ilidaiwa kwamba staa huyo alielezwa kuwa endapo atakwenda kinyume na hukumu hiyo atakuwa amepingana na amri ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo.
Ilidaiwa kwamba staa huyo alielezwa kuwa endapo atakwenda kinyume na hukumu hiyo atakuwa amepingana na amri ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo.
“Kesi ilikuwa ikirindima kwa muda mrefu
kwenye mahakama hiyo lakini hivi karibuni imefikikia tamati,” kilisema
chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini.
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimtafuta Ruge ili kuthibitisha habari hiyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimtafuta Ruge ili kuthibitisha habari hiyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli kesi moja ya kututukana kwenye
mitandao ya kijamii imeshatolewa hukumu na kwa taarifa ni kweli hatakiwi
kuongea chochote juu yetu ila bado kuna kesi nyingine inaendelea,
nafikiri maelezo mazuri zaidi nitakukutanisha na wakili wetu ndiye
atakufafanulia zaidi.”
Mei, 2013, Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jide mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.
Mei, 2013, Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jide mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment