Aliyekuwa
Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa,
amemtaka Rais Dkt. John Magufuli kuifuta kauli yake ya kuwataka wabunge
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasishirikiane na wabunge wa vyama vya
upinzani.
Alizungumza
hayo jana kwenye ziara ya viongozi wa CHADEMA katika mkoa wa Pwani na
Dar es Salaam. Lowassa alidai kuwa kauli hiyo ya Rais Dkt. Magufuli
inabomoa misingi ya amani iliyowekwa na waasisi wa taifa letu.
Alisema “Namuomba
Rais aisahihishe kauli hiyo na nawaomba watanzania tukatae kugawanywa…
Tusikuballi, nchi hii ni yetu sote hakuna mtu mwenye haki miliki hapa.
Ikienda vibaya tutaangamia wote na ikienda vizuri tutafaidi wote,
kwahiyo tukatae.”
Aliongeza
kuwa watanzania wamekuwa wakiishi bila kubaguana kwa misingi ya dini,
rangi au ukabila na kukumbushia kauli iliyowahi kutolewa na baba wa
taifa kuwa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukishakula hutotaka
kuiacha.
Katika
kikao hicho alizungumzia pia juu ya hali ya maisha na uchumi kuwa
mgumu, bei za bidhaa kupanda na mipango mibovu ilivyosababisha sekta
binafsi kuyumba hali iliyosababisha kuongezeka kwa watu wasio na ajira
nchini.
No comments:
Post a Comment