Friday, 17 February 2017

VILOBA KWISHA HABARI YAKE TANZANIA




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuanzia Machi Mosi, mwaka huu Serikali itapiga marufuku pombe kali maarufu kwa jina la ‘viroba’.

Ametoa kauli hiyo wakati akizumgumza na maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara.

“Kuanzia tarehe 1 mwezi 3 ni marufuku kuzaliwa viroba , tutakae mkuta na viroba sisi na yeye, wanaotengeneza pombe watengeneze pombe waziweke katika ukubwa unaokubalika. Sasa hivi viroba
vinatumika kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, watoto wa shule za msingi wanatumia kwa sababu ni rahisi kuweka mfukoni na kutembea navyo.

Hivi karibuni bunge lilijadili suala la usitishaji wa pombe aina ya hiyo na kuahidi lipo katika mchakato.

No comments:

Post a Comment

advertise here