NI
mechi ya vita na kisasi. Ndivyo ambavyo inaweza kutafsiriwa katika
mchezo wa mahasimu wawili Simba na Yanga utakaochezwa leo kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo
huo ni vita kwasababu ndizo timu zinazoongoza kwenye msimamo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara kwa tofauti ya pointi mbili, Simba ikiwa na pointi 51
katika michezo 22 na Yanga ikishika nafasi ya pili kwa pointi 49 katika
michezo 21 iliyocheza.
Aidha,
Simba ina ukame wa mataji ya ligi baada ya kukosa karibu misimu minne
ikizidiwa na Yanga ambao ni mabingwa watetezi wakishinda taji hilo
karibu misimu mitatu mfululizo.
Simba
ambao ndio wenyeji wanahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kubaki
kileleni na kutetea nafasi yao ya uongozi na kuwa rahisi katika mbio za
kusaka ubingwa. Pia, Yanga wanahitaji ushindi kuwa katika nafasi nzuri
ya kutetea taji lao.
Ni
mchezo ambao utatoa taswira nani akayechukua ubingwa msimu huu ndio
maana vita lazima iwepo ya kuwania kupata pointi tatu kwa kila mmoja.
Pia,
ni mchezo wa kisasi kwa vile Simba imeshindwa kutamba mbele ya Yanga
baada ya raundi ya kwanza kutoka sare ya bao 1-1. Pia, msimu uliopita
Simba ilifungwa jumla mabao 4-0, kwa maana ya raundi ya kwanza 2-0 na ya
pili 2-0.
Kwa
ujumla, michezo waliyowahi kucheza ni 92 na kati ya hiyo, Yanga
imeshinda 35 na Simba 25 wakipata sare 32, Yanga ikiongoza kwa magoli
101 na Simba 89.
JIFUNZE ANIMATION TEXT KWA MUDA MCHACHE TU CKECK VIDEO HII
JIFUNZE ANIMATION TEXT KWA MUDA MCHACHE TU CKECK VIDEO HII
Katika
ligi msimu huu mpaka sasa, Yanga inaongoza kwa mabao 46, Simba 36 hivyo
kuonesha wazi kuwa wako vizuri katika safu ya ushambuliaji.
Katika
mabao ya kufungwa Yanga imefungwa tisa na Simba saba, hivyo wekundu hao
wa Msimbazi wako vizuri katika safu ya ulinzi. Katika safu ya
ushambuliaji, Yanga inawategemea Simon Msuva, Obrey Chirwa na Amis
Tambwe.
Pia,
Donald Ngoma ingawa uongozi wa Yanga ulisema unamwandaa kwa ajili ya
mchezo wa kimataifa dhidi ya Zanaco. Simba inawategemea Laudit Mavugo,
Ibrahim Ajib na Shiza Kichuya katika mashambulizi.
Timu hizo zote zinaongozwa na makocha wa kigeni wenye uwezo wa kusoma mchezo na kufanya mabadili ya maana ili kupata matokeo.
Simba
ikiwa na Joseph Omog mwenye uzoefu na mechi hizi tofauti na George
Lwandamina ambaye utakuwa ni mchezo wake wa kwanza wa ligi kukutana na
mahasimu hao ukiacha ule wa Kombe la Mapinduzi Zanzibar walipotoka sare
ya bila kufungana.
Huu utakuwa ni mtihani wa kwanza kwa Lwandamina kukutana na mechi yenye presha ya mashabiki wengi uwanjani.
Mechi
hii inatarajiwa kuchezeshwa na mwamuzi wa kati Mathew Akrama kutoka
Mwanza akisaidiana na Mohamed Mkono wa Tanga na Hassan Zani wa Arusha.
Huyu
ni mwamuzi ambaye hana beji ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA),
lakini amechaguliwa kutokana na aina ya mechi hii yenye presha, kutokana
na uadilifu kwamba anaweza kuchezesha kwa haki kama ambavyo inatarajiwa
na wengi.
NA GRACE MKOJERA
No comments:
Post a Comment