Sunday, 26 February 2017

ILIKUPITA HII YA RIDHIWANI KIKWETE KUKUTANA NA EDWARD LOWASA KWA MARA YA KWANZA IPATE HAPA



Baada ya Jana Ridhiwani Kikwete Kukutana na Edward Lowassa Uwanja wa Taifa na Kupiga nae Stori kidogo amefunguka haya kwenye ukurasa wake wa Twitter:


"Siasa ni Shule ambayo haina kikomo. Tusichoke kujifunza. Mimi nahisi bado niko shule ya Msingi na ninaendelea kujifunza.#siasasivita" Ridhiwani
Mechi ya Simba vs Yanga leo imemalizika kwa ushindi wa Simba kupata goli 2-1 lakini pia imekutanisha baadhi ya viongozi kutoka vyama viwili vya kisiasa Tanzania ambavyo ni CHADEMA na CCM.

Kwenye mechi ya leo aliyekuwa Mgombea Urais 2015 kupitia CHADEMA Edward Lowassa, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe,Khamis Mgeja,Wema Sepetu walikuwa wamekaa eneo moja kutazama mpira na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete na Waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Nape Nnauye na walionekana wakisalimiana.
Wakisalimiana Jamal Malinzi Rais wa TFF, Edward Lowassa na Nape Nnauye
Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya Mashabiki
Mwenyekiti Freeman Mbowe akizungumza na Edward Lowassa

No comments:

Post a Comment

advertise here