Waziri mkuu nchini Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, amejiuzulu na kutoa fursa ya
kuteuliwa mrithi wake kuongoza serikali ya mpito.
Kujiuzulu kwa
bwana Ponyo ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita
kati ya serikali ya Rais Joseph Kabila na baadhi ya vyama vya upinzani
ya kuhairisha uchaguzi wa urais hadi mwezi Aprili mwaka 2018.Wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa muhula wake wa mwisho.
Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.
Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu pamoja na bwana Ponyo.
No comments:
Post a Comment