Thursday, 10 November 2016

MELANIA TRUMP MWANAMITINDO WA KWANZA KUINGIA IKULU

post-feature-imageMKE wa Donald Trump, Melania Trump, anakuwa mwanamitindo wa kwanza kuingia Ikulu ya Marekani baada ya mume wake jana kuchaguliwa kuwa rais wa nchini hiyo.

Shughuli kubwa ya Melania ni pamoja na kushughulikia masuala yanayohusu ustawi wa jamii na familia kwa ujumla.

Hata hivyo, wajibu huo haujabainishwa kuwa rasmi, lakini mke huyo wa rais anatarajia
kuongoza na kuleta ufanisi katika kampeini mbalimbali zinazohusu nyanja hiyo ya ustawi, kuongoza shughuli mbalimbali akiwa ikulu na kumwakilisha rais katika masuala mengine.

Mwanamitindo huyo amemtaka mumewe kuacha matumizi ya mitandao wakati akiwa na nia ya dhati ya kupinga ubaguzi na unyanyasaji kwenye mitandao.

Melania alizaliwa mwaka 1970 nchini Yugoslavia, pia ni mke wa pili wa rais kuzaliwa nje ya Marekani, baada ya Lousia Adams, aliyekuwa mke wa John Quincy Adams, aliyezaliwa England.

Mwanamitindo huyo aliye na umri wa miaka 46, alianza shughuli za mitindo tangu alipokuwa na umri wa miaka 16 na alipofikisha umri wa miaka 18, alisainiwa na wakala wa shughuli hizo mjini Milan, nchini Italy.

Picha yake imepamba majarida mbalimbali yakiwemo ya Harper’s Bazaar, Vanity Fair na Jarida la England la GQ.

Mke huyo wa Trump ana miliki kampuni ya vidani na vipodozi mbalimbali na ana uwezo wa kuzungumza lugha mbalimbali ikiwemo Kislovenian, Kiserbia, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani.

Jinsi alivyokutana na mumewe

Mwanamitindo huyo alikutana na Trump katika wiki ya mitindo jijini New York, Septemba mwaka 1998, baada ya kuachana na mkewe wa kwanza Marla Marples.

Walitangaza uchumba mwaka 2004 na kuoana mwaka 2005 jijini Florida nchini Marekani.

Katika harusi hiyo, mke wa Trump alivaa gauni la harusi lililokadiriwa kuwa na thamani ya Dola 100,000, sawa na 213,820,000 za Kitanzania.

Katika harusi hiyo, Hillary na mumewe Bill Clinton walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa na sherehe ilifanyika katika Hotel ya Mar-a-Lago inayomilikiwa na Trump.

Melania alipata haki za kuishi nchini humo mwaka 2001, baada ya miaka 5 na alipata uraia mwaka 2006,

No comments:

Post a Comment

advertise here