Monday, 26 September 2016

KWA NINI DIAMOND PLATNUMZ NIMEKUWEKEA SABABU ZA UTOP WAKE HAPA

SUBSCRIBE YOUTUBE HAPA
Unadhani kwanini pamoja na kuwa kinywaji na brand maarufu duniani, Coca-Cola inaendelea kumwaga fedha nyingi kwaajili ya matangazo?

Kampuni hiyo hutumia zaidi ya dola bilioni 3 duniani kote kwaajili ya matangazo kila mwaka. Kwanini sasa wanahitaji fedha nyingi kiasi hicho kujitangaza wakati kila mmoja katika dunia hii anaijua Coca-Cola?

Ni hivi – matangazo hayakukumbushi uende kununua soda pale unapokuwa na kiu – lahashaa! Kazi yake ni kuhakikisha jina lake linakaa zaidi kichwani kwako, na ni jina ndilo unalolinunua. Kwahiyo watahakikisha wanajitangaza ili ile nembo ya Coca-Cola ikae daima kichwani kwako.


Mfano huu unahusiana vipi na Diamond? Kwa ukubwa wote alionao, mashabiki wote hao alionao, kwanini bado anaendelea kuzipigia promo ngoma zake kiasi hicho? Kwa hatua aliyofikia, anaweza kuachia wimbo na kutoa link mara moja tu na mashabiki wenyewe wakashughulika nao, lakini hafanyi hivyo. Akitoa wimbo ataupigia promo kwa kuweka post kibao kila siku.

Promo kwa msanii ni kama tu ilivyo matangazo kwa makampuni kama Coca-Cola. Kwahiyo Diamond anafanya kile kile makampuni makubwa yanafanya – kuhakikisha anaijenga brand yake kwenye mawazo yako kiasi ambacho huwezi kumsahau wala kumkwepa.

Hii ndio maana hata video zake zimekuwa zikipata views nyingi kwa muda mfupi na kuwazidi wasanii wengi wakubwa wa Afrika ambao huwa hawasumbuki kupiga promo kubwa kwa nyimbo zao.

Hivyo, ni sahihi kumuita Diamond supastaa anayeutreat muziki wake kama underground. Licha ya ukubwa alionao, staa huyu bado anauchukulia muziki wake kwa mtazamo ule ule msanii mpya huwa anakuwa nao – kwamba hakuna anayenijua hivyo nahitaji kuisukuma zaidi kazi yangu.
Mfano, tangu video yake ya Salome imetoka, ameshapost kwenye Instagram (followers milioni 2.8) picha au video zinazoipromote ngoma hiyo zifikazo 39, katika kipindi cha siku 7 tu! Katika kipindi cha siku 7, ameshapost Facebook (likes milioni 1.6) kupromote wimbo huo, mara 28. Anafanya hivyo Snapchat, anafanya hivyo Twitter pia – kila siku.

Video ya P-Square, Bank Alert imetoka Septemba 18 na sasa hivi na views milioni 1.58, nyuma ya Salome yenye views milioni 2.3 na huku ilitoka siku 2 mbele. Tangu muda huo, Peter Okoye mwenye followers milioni 1.8 Instagram, ameweka post za kuupromote wimbo huo 6 tu!

Simaanishi kuwa kila msanii Afrika anapaswa kufanya kama anavyofanya Diamond, bali nakuonesha jinsi gani anavyochukulia kazi yake kwa mtazamo sawa kama ambavyo kampuni kama Coca-Cola inafanya. Kwamba licha ya ukubwa walionao, wanafanya kazi kwa mtazamo kuwa hakuna anayewafahamu. Ni ngumu kuchuja kwa msanii au kampuni yenye mentality hii.

Fredrick Bundala

No comments:

Post a Comment

advertise here