Friday 20 May 2016

TANZANIA KUCHUANA NA MALAYSYA ULIISKIA HII

LIKE PAGE YETU FACEBOOK  HAPA
https://www.youtube.com/watch?v=a4HLJVd_5to
Timu ya Taifa ya vijana wa Tanzania wa chini ya miaka 17 Serengeti Boys siku ya Jumamosi itacheza na Malaysia kwenye mechi yao ya mwisho ya kundi wakisaka ushindi ili kutinga fainali ya 2016 AIFF Youth Cup huko Tilak Maidan Stadium, Vasco, Goa nchini India.
Tanzania mpaka sasa imeshacheza mechi 3 na kuifunga India 3-1 na kutoka Sare na USA 1-1 na kisha South Korea 1-1.
Ili kutinga Fainali Serengeti Boys wanapaswa kuifunga Malaysia ambayo imetoka sare na India na kubondwa na South Korea 3-0.
Ikiwa Serengeti Boys wataifunga Malaysia basi njia yao itakuwa nyeupe ikiwa pia Jumamosi mechi kati ya Marekani na Korea Kusini itaisha kwa timu moja kushinda.
2016 AIFF Youth Cup ni mashindano yaliyoandaliwa na shirikisho la soka la India, All India
Football Federation (AIFF), mahsusi kuitayarisha Timu yao ya U-17 kwa ajili ya mashindano ya AFC U-16 na yale ya 2017 FIFA U-17 World Cup.
Mashindano haya yanachezwa kuanzia Mei 15 hadi Mei 25 huko Tilak Maidan Stadium huko Vasco, Goa nchini India,mashindano haya yana hatua mbili za kundi na za mtoano.Timu 4 za juu za kundi ambalo lina timu 5 zitasonga kuingia mtoano ambapo timu mbili za juu zitacheza fainali.
EBANA EEE KILIKUPITA KI CHEKESHO HIKI

No comments:

Post a Comment

advertise here