KUNDI LA MAUAJI RWANDA NAIBU KAMANDA MIKONINI MWA SHERIA
LIKE US ON FACEBOOK
Bofya picha hii kujiunga na bztv online Mpiganaji wa kundi la FDLR
Wakuu wa Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo wanasema wamemkamata naibu kamanda wa kundi la
wapiganaji, linalohusishwa na mauaji makubwa ya Rwanda ya mwaka 1994.
Msemaji
wa serikali, alieleza kuwa Jenerali Leopold Mujyambere, wa kundi la
Rwanda la FDLR, alikamatwa mjini Goma, mashariki mwa nchi.
Kundi la FDLR ni la Wahutu wanaoshutumiwa kuuwa malaki ya Watutsi na
Wahutu waliokuwa na msimamo wa wastani, wakati wa mauaji ya kimbari ya
Rwanda.
Rwanda imeingilia kati kijeshi mashariki mwa Congo katika juhudi za kuliangamiza kundi hilo.
No comments:
Post a Comment