Monday 18 April 2016

TP MAZEMBE IPO HOI DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

LAYIII

Mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa Afrika katika kandanda klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco katika jitihada zake za kuhifadhi taji lao.
Mabingwa hao wa Afrika wanahitaji kushinda Wydad kwa zaidi ya mabao mawili na wasifungwe lolote ilikunusuru hadhi yao baada ya o kuchapwa 2-0 katika mkondo wa kwanza Juma lililopita .
Mazembe inawakaribisha mabingwa hao wa Morocco katika mkondo wa pili jumatano hii.
Hii ndio itakayokuwa mara ya kwanza kwa mechi za klabu bingwa kuchezwa katikati ya juma.
Mshindi wa mechi hiyo atafuzu kwa mkondo wa pili.

Hapo kesho, Alex McLeish ataiongoza Zamalek ya Misri kutetea uongozi wa mabao mawili kwa nunge dhidi ya Mouloudia Bejaia ya Algeria.
Aidha Zesco United ya Zambia inaialika Stade Malien ya Mali.
Zesco iko kifua mbele kwa mabao 3-1.
Vile vile mabingwa wa mwaka wa 2014 Entente Setif, ya Algeria waliotoka sare ya 2-2 na Al Merreikh katika mkondo wa kwanza sasa wanawapokea mabingwa hao wa Sudan.

No comments:

Post a Comment

advertise here