LAYIII
Asubuhi ya March 9 taarifa za ajali kutokea maeneo ya Tabata Dar Es Salaam zilisambaa katika sehemu mbalimbali hususani, katika mitandao ya kijamii. Tabata ilitokea ajali iliyokuwa inahusisha basi la abiria aina ya DCM, tipa la mchanga na Lori la ng’ombe.
Ajali hiyo imekuwa ikiripotiwa kuchukua uhai wa watu kadhaa na majeruhi ila taarifa zaidi zinasubiriwa kutolewa, ripota wa millardayo.com alipita kituo cha Polisi Buguruni na kukuta umati umekusanyika na kushangaa DCM ilivyoharibika, ambayo ipo kituoni hapo muda mrefu, lakini watu bado hawaamini kilichotokea.
No comments:
Post a Comment