Sunday, 20 March 2016

KIZUNGU CHA SHILOLE CHA KADILIWA KUMPA MASHABIKI WENGI KATIKA ANGA ZAKE ZA MZIKI

LAYIII
Kwa utafiti uliofanyika na swaxbz.com inaonekana kwamba kama shilole ataendelea kutumia swaga zake za uongeaji wa kizungu chake cha kuchekesha chekesha basi itamsaidia sana kumpa kiki na kuufanya mziki wake uendelee kukua.
BONYEZA PICHA UJICHEKEE MWENYEWE KIZUNGU ANACHOTUMIA SHILOLE AKIWA KATIKA MATAMASHA YAKE NDANI NA NJE YA NCHI
show flani amizing aliyowahi kuifanya shilole
 https://www.youtube.com/watch?v=iAzdoV5TW1Y
Msanii Shilole au Shishi Baby, anatafuta mwalimu wa kumnoa kwenye lugha ya kingereza, ikiwa ni maandalizi ya kuonana na msanii wa Marekani Nicki Minaj.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Shilole amendika tangazo akimtaka mtu ambaye ni mwalimu wa lugha hiyo kuwasiliana, ili aweze kuanza mafunzo hayo.

“Anatafutwa mwalimu wa kingereza mzuri, jamani huu sio utani nipo sirias naona hali ishakuwa sio hali soon natakiwa kuonaa na Niki Minaji hivyo lazima nijinoeee, namba ya sm 0653883839”, aliandika Shilole kwenye ukurasa wake wa instagram
Shilole anafahamika kwa kutojua lugha ya kingereza, hivyo kuwa gumzo anapoongea lugha hiyo ambayo mara kwa mara huwa anachapia, lakini cha ajabu yeye mwenyewe huwa anafurahia na hajutii kuzungumza lugha hiyo ambayo haijui, kama alivyowahi kutamka neno la “I love is my country”, ambalo lilikuwa maarufu na watu kuvutiwa nalo.


No comments:

Post a Comment

advertise here