Tuesday 15 March 2016

JE KUNA UKWELI KUHUSU RAIS MAGUFULI KUWAPUZIA MARAIS WASTAAFU ULINZI ........ UKWELI WOTE HAPA

LAYIII
Kwenye Gazeti la JamboLEO, toleo namba 2381 la tarehe 15 March 2016 limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho Magufuli awapunguzia ulinzi marais wastaafu
Taarifa yake kamili ipo katika ukurasa wa nne na inaeleza kuwa Rais Magufuli amewapunguzia
ulinzi Marais wastaafu na imewataja marais hao kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.
Jamboleo
Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa taarifa hizo sio za kweli na inalitaka gazeti hilo kukanusha habari hiyo mara moja, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Taarifa iliyotolewa kupitia kwa kaimu mkurugenzi wa mawasiliano, IKULU Gerson Msigwa ni kwamba pia IKULU inasisitiza kwamba Watanzania wanatakiwa kufahamu kuwa utaratibu wa ulinzi wa Marais wastaafu haujabadilishwa.


No comments:

Post a Comment

advertise here