LAYIII
VIDEO BONYEZA PICHA HIII
VIDEO BONYEZA PICHA HIII
Stori: Musa Mateja, Wikienda
DAR ES SALAAM: Kutoka Tandale hadi
Marekani! Staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
melidokezea Ijumaa Wikienda kilichojiri kwa takriban dakika 20
alipokutana uso kwa uso na rapa kubwa duniani wa Marekani, Kanye West.
UWANJA WA NDEGE LOS ANGELES
Diamond alikutana na Kanye West kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Los Angeles wa LAX nchini Marekani
wakati akisubiri ndege kuelekea Las Vegas kwa ajili ya shoo na kazi zake
za kimuziki.
Katika mahojiano maalum na Ijumaa
Wikienda akiwa Las Vegas, Diamond alisimulia alivyokutana na Kanye West
na kufanikiwa kuzungumza naye tofauti na watu wengi wanavyoamini kuwa
jamaa huyo siyo mtu wa ‘kuingilika’ kirahisi.
MAHOJIANO
Wikienda: Ilikuwaje ukaweza kupiga picha na Kanye West?
Diamond: Dah! Aisee ni kama zali vile
maana sikuamini kama ni mimi mtoto wa Kimanyema nipo na Kanye West.
Kwanza nilipomuona nilishtuka sana lakini nikasema piga ua, liwalo na
liwe ngoja nimvae pamoja na kwamba alikuwa na timu ya kufa mtu.
Wikienda: Hukuzuiwa kumfuata na kumvaa
kwa sababu tunavyojua huwa ana mabaunsa na mtu haruhusiwi kumsogelea
hadi akubali mwenyewe?
Diamond: Kiukweli ilikuwa kazi sana
lakini niliwafuata watu wake wakiwemo mameneja wake, nikajitambulisha
ndipo wakamwambia akaitikia nimsalimie na kuongea naye.
MAZUNGUMZO DAKIKA 20
Wikienda: Mazungumzo yenu yalichukua muda gani na mlizungumza kuhusu nini?
Diamond: Tulitumia kama dakika 20 na
zaidi kwa sababu naye alikuwa anasubiri ndege lakini hasa ilikuwa ni
kujitambulisha, kuwaonesha kazi zangu kwenye YouTube na kuweka mipango
ambayo ni mapema mno kuiweka wazi.
Wakati nauanza mwaka huu nilisema kuwa kwa Afrika muziki wetu wa Bongo Fleva umeeleweka na mwaka huu ni zamu ya
Marekani na kweli naona milango inaanza kufunguka.
Wikienda: Unaweza kudokeza angalau kidogo mlichokubaliana?
WABADILISHANA MAWASILIANO
Diamond: Kwanza ilikuwa ni kufahamiana kisha nilibadilishana naye mawasiliano hivyo naamini mambo mazuri yanakuja.
Zaidi sana ni kuhusu muziki wetu na namna ya kujipanua kibiashara.
Wikienda: Ilikuwaje akakubali upige naye picha?
Diamond: Wakati anaondoka kwa sababu alionekana kuwa na haraka, niliwaomba mameneja wake, wakaniruhusu, si unajua tena?
Nikachomoa simu yangu fasta na kugonga naye picha. Cha msingi tuombeane Mungu mambo yaende sawia.
Wikienda: Mbali na kufanikiwa kukutana na Kanye West, una program gani nyingine huko?
Diamond: Kwanza nina shoo hapa Las Vegas
kisha nitafanya video ya ngoma yangu mpya na Ne-Yo (mwanamuziki wa
Marekani) ambayo tayari tulishafanya audio.
WABONGO WENGINE NA KANYE WEST
Mbali na Diamond, mastaa wengine wa
Kibongo waliowahi kukutana na Kanye West na kupiga naye picha ni sexy
lady wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee na mwanamitindo Miriam Odema.
No comments:
Post a Comment