Saturday, 13 February 2016

ZARI AKUTANA NA ISSUE YA KUWA NA MAKALIO FEKI

LAYIII

zariNasibu Abdul ‘Diamond’ na mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari’
Stori: Musa mateja, Ijumaa
Dar es Salaam
Mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ukipenda muite mama Tiffah, amekwaa skendo ya kutumia makalio feki kila anapokuwa kwenye mtoko.

Zarimond
Mjadala wa muonekano wa Zari ulianzia siku alipomsindikiza Diamond kusaini mkataba mnono wa Kampuni ya Vodacom ambapo akiwa amevalia kigauni chake chekundu, alionekana kuwa na ‘zigo’ kuliko alivyozoeleka.
Licha ya siku hiyo Zari kuwashangaza wengi, mjadala ukahamia kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya wadaku walitupia picha za hivi karibuni zinazomuonesha akiwa hajajaladia kisha kuunganisha na ile aliyovaa kigauni chekundu akiwa amekumbatiwa na Diamond.
Hata hivyo, wengi walioziona picha hizo walitilia shaka mzigo aliokuwa nao Zari siku hiyo na kuishia kusema kuwa, huenda kila akitoka anavaa makalio feki ambayo wanawake wengi wa mjini huyatumia.
“Haya siyo orijino, Zari namjua vizuri, hili kalio ni feki, itakuwa kila akitoka anajaladia,” alisema mmoja wa wadau aliyejitambulisha kwa jina la Zahara.
zari8Kufuatia mjadala kuwa mkubwa, juzi Zari alivunja ukimya na kueleza kuwa, wala hatumii makalio hayo feki bali umbile lake ni orijino na hajabadilika tangu alipokuwa mjamzito, alipojifungua na alivyo sasa, kisha akatupia picha mbalimbali zinazomuonesha makalio yake.
“Huwa situmiagi hayo makalio feki, umbile langu ni orijino kabisa ona tangu nikiwa na ujauzito mpaka leo hii,” alisema Zari.
Naye Diamond alipozungumza na Ijumaa kuhusiana na mzazi mwenzake huyo kutuhumiwa kutumia makalio feki alisema: “Mimi namjua vizuri Zari kuliko mnavyomjua, kama ni zigo, ni orijino. Watu wanashindwa kuangalia mtu kapozi vipi na kavaa nini kwani hayo yanabadilisha muonekano wa mtu.”

No comments:

Post a Comment

advertise here