MTOTO WA SOKWE ANAENDELEA VIZURI BAADA YA KUZALIWA KWA UPASUAJI
LAYIII
Mwana wa Sokwe anaendelea vyema baada ya kuzaliwa kupitia upasuaji katika hali isiyo ya kawaida.
Sokwe huyo anayetoka upande wa magharibi alizaliwa kupitia upasuaji
usio wa kawaida baada ya mamaake kuonyesha ishara za ugonjwa hatari wa
shinikizo la damu.
Alihitaji msaada wa kupumua,lakini sasa madaktari wanasema hali ya mama na mtoto iko shwari.
CHUKUA MUDA WAKO KUITAZAMA VIDEO HII YA MAGARI YANAYOTEMBEA NDANI YA MAJI
Kumekuwa na sokwe wachache waliofanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua
duniani,kisa cha hivi majuzi kikiwa kile cha San Diego Safari Park
mwaka 2014.
Sokwe huyo aliye na siku 11 alizalishwa na Professa David Cahill
ambaye amewazalisha wanawake wengi kupitia upasuaji ,lakini ilikuwa mara
yake ya kwanza kumzalisha sokwe.
”Mbali na kuwa na watoto wangu,huu ni ufanisi mkubwa kwangu,kitu ambacho sitoweza kusahau tena,”alisema.
Aliulizwa maoni yake baada ya mamaake sokwe huyo kwa jina Kera kuugua ugonjwa wakati ambapo alikuwa karibu kujifungua.
Chanzo: BBC.
No comments:
Post a Comment