Thursday, 4 February 2016

KAMA HUJUI ANAYE FATA KATIKA YALE MAJIPU YANAYOTUMBULIWA SOMA HAPA

LAYIII

Magufuli3 (1)Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’.
Stori: Gabriel Ng’osha, Wikienda
Dar es Salaam: Who is next (nani anafuatia?) Ndivyo Wabongo wengi wanavyojiuliza kufuatia tumbutumbua majipu katika sekta za serikali inayofanywa na Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ ili kupisha mfumo mpya wenye Kauli Mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.
Kwa mujibu wa baadhi ya wananchi waliozungumza na Ijumaa Wikienda kwa nyakati tofauti, wana imani na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ kuwa hatanii katika suala la tumbuatumbua ya majipu inayoendelea ambapo familia za wakurugenzi waliotumbuliwa sasa ni vilio tupu.

Kwa kujali afya za wananchi wake, mara tu baada ya kuingia ikulu na kupata mamlaka ya kisheria alianza na;
hussein-kidanto-surgeon-987Dk Hussein Kidanto
MUHIMBILI
Baada ya rais kuitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kubaini madudu mengi ikiwemo ubovu wa mashine za kupima wagonjwa za CT- SCAN na MRI kwa takriban miezi kadhaa, aliamua kumsimamisha mkurugenzi wake, Dk Hussein Kidanto na kufuta bodi ya afya ambayo ilikuwa imemaliza muda wake.
Rished BadeRished Bade
TRA
Haikuishi hapo, Rais Magufuli akamsimamisha kazi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade kufuatia kasoro kubwa za kiutendaji zilizobainika katika mamlaka hiyo hasa suala la ukusanyaji kodi.
Tiagi MasamakiTiagi Masamaki
FORODHA
Rais Magufuli hakuishia kwa Bade, rungu likahamia kwa Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Tiagi Masamaki ambaye naye kibarua kiliota nyasi kwa tuhuma kadha wa kadhaa ikiwemo ya makontena yaliyopotea bandarini chini ya usimamizi wake.
hosea
Dk. Edward
TAKUKURU
Mwingine aliyekutwa na tumbuatumbua majipu ya Rais Magufuli ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hosea ambaye naye alisimamishwa kutokana na rais kutokuridhishwa na utendaji kazi wa taasisi hiyo.
Benhadard Tito
Mhandisi Benhadard Tito
RAHCO
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito naye alisimamishwa kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.
directorAugustino Kalinga
MANISPAA YA DODOMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Augustino Kalinga yeye alitumbuliwa jipu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene kupitia Serikali ya Rais Magufuli kufuatia kuruhusu ofisi yake kuchangisha wazazi michango ya elimu ya msingi ilihali serikali imekataza na kutamka kuwa sehemu ya elimu itatolewa bure.
Awadhi MassaweAwadhi Massawe
BANDARI
Hii ni Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambapo Rais Magufuli alimtimua Mkurugenzi Mtendaji, Awadhi Massawe na kuvunja Bodi ya TPA kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Anga-21Charles Chacha
MAMLAKA YA ANGA
Serikali ya Rais Magufuli kupitia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mabarawa ilimsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Charles Chacha na kutaka kuhamishwa mara moja kwa Mhasibu Mkuu, Alhaji Said Mteule na Meneja Manunuzi, Said Kaswela kwa kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato.
John WangaJohn Wanga
MKURUGENZI ILEMELA
Wakati mambo yakiwa moto, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Suleiman Jaffo, naye alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Mwanza, John Wanga kutokana matumizi mabaya ya madaraka.
Sylvester-AmbokileSylvester Ambokile
UHAMIAJI
Hii ni moja ya idara nyeti ambayo ilibainika kuwa na madudu baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kuitembelea, jambo lililomlazimu Rais Magufuli kumsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile kupisha uchunguzi katika idara hiyo iliyogubikwa na tuhuma za rushwa, ukusanyaji mbaya wa maduhuli ya serikali, ukiukwaji wa taratibu za manunuzi na utendaji mbovu.
Wakili Heche Suguta ManchareWakili Heche Suguta Manchare
NEMC
Mmoja wa waliosimamishwa katika idara hii ni Mwanasheria Daraja la II Wakili Heche Suguta Manchare na wenzake huku wakituhumiwa kukiuka miiko ya kazi yao katika kusimamia kiwanda cha kusindika minofu ya punda kilichopo mkoani Dodoma.
DSC_0092Mussa Natty
KINONDONI
Tumbuatumbua pia ilimfika Mhandisi, Mussa Natty aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma ya usimamizi mbovu wa barabara, ubinafsishwaji wa Ufukwe wa Coco na migogoro ya ardhi.
Dickson MaimuDickson Maimu
NIDA
Pia hivi karibuni rungu lilitua kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na watendaji wengine wanne ambao walisimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa matumizi ya Sh. bilioni 179.6 huku zoezi la uandikishwaji na utolewaji wa vitambulisho likilalamikiwa na Watanzania wengi. Swali ni je, Who is next

No comments:

Post a Comment

advertise here