Sunday, 6 December 2015

ULIPITWA NA KISA CHA MWANAMKE ALIYEMWAGIWA MAJI YA MOTO KISA WIVU WA MAPENZI BONYEZA LINK

LAYIII
Bonyeza picha hii kuiona video yake
20131213-141212.jpg
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu akipata matibabu hospitalini.
20131213-140854.jpg
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

20131213-140556.jpg
Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.
cheka kidogo
MWANAMKE mmoja mkazi wa Mbuguni Arusha,Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kisa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.
Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru alikolazwa,Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma lililopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka afike nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kumwagia maji ya moto.
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la madaktari hospitalini hapo. Naye Muuguzi wa wodi ya majeruhi Mount Meru Hospitali Bi. Neema Bayo amesema matukio kama hayo yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali nchini, bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini.
Ofisa wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha, Maria Maswa akizungumza wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika hospitali ya mount Meru, amesema yanapotokea matukio hayo, walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo hayo. Maria Maswa – Ofisa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema “Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi Novemba 2012 mpaka sasa.


No comments:

Post a Comment

advertise here