Thursday, 12 November 2015

EDWARD LOWASSA JUKWAANI TENA ARUSHA AWATISHIA VIGOGO

LAYIII
Good Morning mtu wangu asubuhi yako inaendaje? Inawezekana uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita, pengine ulikuwa busy na hukuzipata zote kwenye kuperuzi na kudadis redioni ila nilizozirekodi zote ziko hapa.
Wajawazito wafichua madudu ya hospitali ya mkoa wa Arusha, Mt. Meru baada ya kukosa vipimo muhimu kama Ultra-sound na hivyo kulazimika kwenda hospitali binafsi ili kupata huduma hiyo, vita
dhidi ya ujangili inazidi kupamba moto baada ya majangili kumi na mbili kutiwa mbaroni baada ya kukutwa na silaha nzito za kivita, bunduki 3, risasi kadhaa na meno mawili ya tembo.
Aliyekuwa mgombea Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa anatarajia kupanda jukwaani jumamosi hii kumuombea kura Mgombea Ubunge wa CHADEMA jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema… Dk. Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema tatizo linalotokea Zanzibar sasa hivi ni zaidi ya Uchaguzi hivyo wakae na kumaliza tatizo hilo wenyewe na sio kukaa na kuwasubiri watu wa nje waje kuwaletea suluhisho.
CHUKUA MUDA WAKO KIDOGO KUANGALIA NGUVU ALIYOKUJA NAYO MAGUFULI KATIKA CRIP HIZI Mamlaka ya mapato Tanzania, TRA imesema kuanzia sasa inaanza kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kuwakamata wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na kuwaweka hadharani pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
Mwenyekiti wa BAWACHA wilaya Arusha, Happy Charles ametishia kuongoza wanawake kutembea uchi barabarani endapo tume ya taifa NEC kwa kushirikiana na CCM watawapora ushindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Arusha mjini.
Kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast bonyeza play hapa chini kwenye hii sauti.


No comments:

Post a Comment

advertise here