LAYIII
Kwenye list ya Wanasiasa walioamua
kuingia kwenye Mchakato wa Uchaguzi Mkuu Tanzania utakaofanyika October
2015, alikuwepo pia Mwanasiasa Mkongwe, Mchungaji Christopher Mtikila ambaye alitangaza kugombea nafasi ya Urais kupitia Chama cha Democratic Party (DP).
October 04 2015 taarifa zimetufikia kuhusu msiba wake, Mchungaji Mtikila amefariki baada ya kupata ajali ya gari ndogo eneo la Chalinze akiwa na watu wengine watatu ambao wamepata majeraha.
Tayari ninazo picha kutoka Mikocheni Dar es Salaam, nyumbani kwa Marehemu Mchungaji Mtikila.. ndugu, jamaa na watu wengine wameanza kukusanyika kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine za Msiba.
Taratibu za Msiba mpaka hatua ya mazishi zote nitakuwa nakusogezea kila zinaponifikia… #RIPMchungaji MTIKILA.
No comments:
Post a Comment