LAYIII
Ahmed Mohamed
ni kijana wa miaka 14, alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kufanya
ubunifu ambao yeye alidhani itakuwa ni kitu kizuri kuwafurahisha Walimu
wake, lakini baada ya kuwaonesha tu ubunifu wake, ikapigwa simu Kituo
cha Polisi na wakamkamata !!
Ahmed ni mwanafunzi wa MacArthur High School
iliyoko Irving, Texas Marekani… ni kijana ambae ana kipaji cha kufanya
ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali nyumbani kwao, alienda Shule na
kisanduku kidogo ambacho alikifanyia ubunifu na kubadilisha kisanduku
hicho kuwa saa.
Walimu walipomkuta na kifaa hicho
walitoa taarifa Polisi, wakamkatamata ili akatolee maelezo vizuri kuhusu
hiyo saa yake… kilichowashtua Walimu ni nyaya nyingi kwenye huo ubunifu
wa saa, Polisi wanasema huenda huyo mtoto akafunguliwa mashtaka ya
kutengeneza bomu feki na kuwatisha watu !!
Ahmed
amesema Polisi wamemhoji kwa nini ametengeneza Bomu? lakini
amewasititizia mara zote kwamba kile kifaa sio Bomu ila ni saa ambayo
aliibuni mwenyewe.
Polisi walimwachia huku uchunguzi
ukiendelea lakini baba yake anaonekana kukasirishwa sana huku akihisi
kwamba kuna ishu ya ubaguzi wa Kidini kwenye suala la mtoto wake
kukamatwa kwa tuhuma hizo… Hii hapa Video ya Ahmed akijieleza ilivyokuwa.
No comments:
Post a Comment