LAYIII
MWANANCHI
Mbunge wa Kahama, James Lembeli ameiweka njiapanda CCM baada ya kutangaza kutogombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
Uamuzi wa Lembeli umekuja wakati
wanachama kutoka sehemu mbalimbali wakitangaza uamuzi wao wa kujiengua
CCM na kujiunga na vyama vya upinzani, hasa Chadema ambayo imesomba
asilimia kubwa ya wahamaji hao.
LEMBELI kuihama CCM?, Mafuriko ya LOWASSA CHADEMA na Mwinyi avunja ukimya…#MAGAZETINI JULY19
MWANANCHI
Mbunge wa Kahama, James Lembeli ameiweka njiapanda CCM baada ya kutangaza kutogombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
Uamuzi wa Lembeli umekuja wakati
wanachama kutoka sehemu mbalimbali wakitangaza uamuzi wao wa kujiengua
CCM na kujiunga na vyama vya upinzani, hasa Chadema ambayo imesomba
asilimia kubwa ya wahamaji hao.
Lembeli alisema taarifa hizo ni uvumi uliozagaa jimboni kwake, lakini hajajiunga na chama chochote.
“Ni
uvumi tu na uvumi wenyewe umechangiwa na swali nililoulizwa leo na
wananchi kwamba ‘mbona toka mchakato wa kuchukua fomu umeanza
hatujakuona’ na mimi nikawajibu kuwa ‘sitachukua fomu’,” alisema.
Lembeli alisema amechukua uamuzi huo
kutokana na rafu inayoendelea jimboni humo na maneno ya baadhi ya
wanachama, wakiwemo viongozi kuwa hatakiwi na vigogo ndani ya CCM.
Lembeli, mmoja wa wabunge waliokuwa
mstari wa mbele wakati wa kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya
Tegeta Escrow, alisema sababu za kutotakiwa huko zinatokana na dhana
potofu ya baadhi ya viongozi kwamba michango yake ndani na nje ya Bunge
inaivua nguo Serikali.
“Tangu
mchakato wa uchukuaji wa fomu umeanza baadhi ya wanachama wengi tu
wameitwa kwenye vikao visivyo halali karibu kata zote wakiwa na kadi zao
na kuorodheshwa na kupewa maagizo ya kunikataa kwenye kura ya maoni na
wengine wanapewa Sh5,000,” alisema mwandishi huyo wa habari.
Lembeli alidai kuwa mbaya zaidi ni
kwamba zipo kadi mpya za CCM zinazotolewa kiholela bila kufuata
utaratibu na licha ya kulalamikia hali hiyo hakuna hatua
zilizochukuliwa.
Alisema kutokana na yote hayo, aliwahi
kusema kwenye mkutano wa hadhara kuwa kuna njama hizo, lakini badala ya
CCM kufanyia kazi madai hayo, wakamuita mbele ya Kamati ya Maadili.
“Kwenye
kamati ya maadili nilituhumiwa kuwa nakidhalilisha chama na kutakiwa
niwataje nani walioniambia sitakiwi. Niliwajibu, tena kwa maandishi na
kuwapa orodha, lakini mpaka leo kimya ina maana mimi bado ni mtuhumiwa,” alidai.
“Mimi
siyo mtoto mdogo. Naelewa nini kinaendelea na ndiyo maana nimesema
sitachukua fomu ya kugombea ubunge kwa mazingira haya. Bado sijatangaza
kuhama CCM”.
Wakati Lembeli akisisitiza suala la
kuhama kwake ni fununu tu, habari nyingine zilidai huenda akagombea
ubunge kwa tiketi ya Chadema kutokana na kutokubaliana na mchakato huo
anaodai ni batili.
MWANANCHI
Janeth Magufuli bado
anasubiri miezi mitatu ya kampeni nzito za kumuwezesha mumewe kuingia
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, lakini walimu na wanafunzi wa Shule ya
Msingi Mbuyuni tayari wanasikitika kumpoteza mwalimu huyo wa jiografia,
historia na Tehama.
Mumewe, Dk John Pombe Magufuli
amepitishwa zaidi ya wiki moja iliyopita kuwa mgombea urais wa Tanzania
kwa tiketi ya CCM, na hivyo atalazimika kupambana vikali na wagombea wa
vyama vingine ili kujihakikishia anaingia Ikulu kuongoza Serikali ya
Awamu ya Tano.
Lakini walimu na wanafunzi wa shule hiyo
wanaona kuwa tayari Dk Magufuli ameshajihakikishia tiketi ya kuingia
Ikulu na walichonacho sasa ni kusononeka kwa kuwa wanampoteza mmoja wa
walimu bora shuleni hapo.
“Kama
mumewe akichaguliwa, nitakosa utu na busara zake. Na unajua? Ni mwalimu
wa mazingira na anajua majukumu yake. Darasa la tano watamkumbuka
sana,” anasema mwalimu mkuu wa shule hiyo, Dorothy Malecela.
“Ni
mwanamke mchapakazi sana na ni mwalimu mzuri, mtu mwenye upendo na
mnyenyekevu. mtu pia mwenye moyo mzuri. Wakati fulani alitoa msaada wa
baiskeli kwa mwanafunzi mlemavu shuleni hapa.”
Alikuwa akimzungumzia mwanafunzi mlemavu Elisha Lameck, ambaye alikuwa akipata shida kutoka sehemu moja kwenda nyingine wakati akiwa shuleni hapo.
Mwalimu Malecela anasema licha ya kuwa ni mke wa Waziri Magufuli, ilikuwa kazi kufahamu kama ni mke wa kigogo.
“Hakuwa na makuu hata kidogo, hata watoto wake walikuwa wakisoma hapa, na mwingine anasoma shule ya Kata ya Oysterbay,” anaeleza.
“Watoto wao wanasoma shule za kawaida sana. Shule ya kata tofauti na wengine ambao huwapeleka nje ya nchi.”
MWANANCHI
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa shughuli ya kupata mgombea urais kwa tiketi ya CCM haikuwa rahisi na akashukuru kwamba imemalizika kwa amani.
Mchakato huo ulihitimishwa Julai 12 mjini Dodoma wakati Mkutano Mkuu wa CCM ulipopitisha jina la Dk John Magufuli kugombea nafasi ya kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake mwishoni mwa mwaka.
Jumla ya makada 38 walijitokeza kuwania
nafasi hiyo, na majina matano ndiyo yaliyopitishwa kwenda Halmashauri
Kuu na baadaye matatu kwenda Mkutano Mkuu.
Mchakato wa urais ndani ya CCM ambao kwa
kawaida hutawaliwa na msuguano kabla ya kumalizika kwa maridhiano,
safari hii ulienda mbali zaidi baada ya wajumbe watatu wa Kamati Kuu
kupinga nje ya kikao uamuzi wa chombo hicho na baadaye wajumbe wa
Halmashauri Kuu kumwimbia mwenyekiti wao, Jakaya Kikwete wimbo wa
kuonyesha wana imani na Edward Lowassa baada ya jina la mbunge huyo wa
Monduli kuenguliwa na Kamati Kuu.
Jana, akitoa hotuba fupi baada ya
kumalizika kwa sala ya Eid el Fitr kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam, Mwinyi alizungumza kwa mara ya kwanza hadharani kuhusu
mchakato huo, akidokeza hali ilivyokuwa.
“Haikuwa kazi rahisi kwenye mchakato huu wa kumtafuta mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya CCM,” alisema Mwinyi lakini akawahi kuipoza kauli hiyo kwa kuelezea amani ilivyotawala mwishoni.
“Kama ni jahazi basi sasa tunashukuru limefika pwani salama.”
“Uchaguzi
huu ni kwa ajili ya kuwapata viongozi wetu, tunataka viongozi bora wa
kutuletea maendeleo, mapatano na wenye mahaba na wananchi.”
Akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza
baada ya mchakato huo wa kumtafuta mgombea wa urais kukamilika mjini
Dodoma, Mzee Mwinyi alimshukuru Mungu kwa mchakato huo kuisha salama.
“Haikuwa
kazi rahisi kwenye mchakato huu wa kumtafuta mgombea mmoja atakaye
peperusha bendera ya CCM, kama ni jahazi basi sasa tunashukuru limefika
pwani salama.
“Sasa, ninawaomba Watanzania kuwa watulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi wa nchi tunaoufanyika kila baada ya miaka mitano,“ alisema
Rais Mwinyi ambaye alikuwa mmoja ya wajumbe wa Baraza la Ushauri
waliofanya kazi ya kutuliza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM hadi
kuafikiana kuendelea na mchakato wa kumpata mgombea urais.
Aliwasisitizia Watanzania kuacha tabia
ya kupenda mno na kuacha kubaguana, akisema hakuna aliye bora na
kuwataka kuzidisha mapenzi miongoni mwao na kusherehekea vyema Sikukuu
ya Eid el Fitr. “Hakuna jambo
lenye maana kama hili la kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye kutufikisha
salama siku kama hii ya leo (jana) ambayo tunasherekea Sikukuu ya Eid,” alisema Mwinyi.
Awali Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Alhad Mussa Salum aliwasisitizia wananchi umuhimu wa kusherekea sikukuu
hiyo katika hali ya amani na utulivu.
Pia, aliwashauri wazazi na walezi
kuwapeleka watoto wao sehemu zenye maadili ili washerehekee kama ambavyo
Mwenyezi Mungu anapenda.
MWANANCHI
Mwigizaji maarufu wa tamthilia ya Isidingo The Need, Jack Devnarain maarufu kwa jina la uigizaji la Rajesh Kumar, amefanikiwa kufika kilele cha Uhuru cha Mlima Kilimanjaro.
Rajesh, ambaye ni raia wa Afrika Kusini,
pamoja na wenzake 36 walipanda mlima huo kuanzia Julai 14, kuadhimisha
siku ya kuzaliwa kwa Hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini.
Mbali na kuadhimisha siku hiyo muhimu
kwa Taifa la Afrika Kusini, pia walipanda kwa ajili ya kuchangisha fedha
za kusaidia afya za watoto wa kike 272,000 wa nchi hiyo na Tanzania.
Mratibu wa Taasisi ya Mandela ya Trek4 Mandela nchini, Honest Minja alisema jana kwamba Kumar na wapanda mlima wenzake 31 kati ya 37 walifanikiwa kufika kileleni.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Erastus Lufungulo alisema kati ya watu 37 waliopanda mlima, 32 walifika kileleni na watano waliishia njiani.
“Wageni
32 wa Trek4 Mandela wamefika kileleni akiwamo msanii wa Isidingo.
Watatu waliishia kituo cha Kibo na wawili waliishia kati ya Kibo na
kilelele cha Gilmans,” alisema.
Kundi hilo la wapanda mlima
lilimjumuisha mpanda milima wa kimataifa Sibusiso Vilane ambaye ni
Mwafrika wa kwanza kupanda mlima Everest ambao ni mrefu kuliko yote
duniani.
Jana walitarajiwa kushuka hadi Kituo cha
Horombo kilichopo urefu wa mita 3,720 na leo walitarajiwa kushuka hadi
Mandara mita 2,700 na baadaye hadi lango kuu la Kinapa lililopo Marangu.
NIPASHE
Shughuli za usafirishaji jana zilisimama
kwa zaidi ya saa mbili, baada ya msafara wa mgombea Urais kupitia Chama
Cha Mapinduzi(CCM), Dk. John Pombe Magufuli, kupita jijini hapa.
Licha ya kusimama kwa usafiri, msafara
huo pia ulizuiwa kwa muda na wananchi katika eneo la Pasiansi, Kona ya
Bwiru na Makongolo, wakishinikiza kusalimiana na mgombea huyo.
Magufuli ambaye aliongozana na viongozi
mbalimbali wa CCM, serikali, madhehebu ya dini na wananchi wengine
kutoka ndani na nje ya mkoa wa Mwanza alitua Uwanja wa Ndege saa 7:50
mchana.
Baadhi ya viongozi wa CCM taifa
waliokuwa wameongozana na Dk. Magufuli ni pamoja na Katibu wa Siasa na
Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho
Tanzania Bara, Rajabu Luhavi.
Kadhalika, Dk. Magufuli alikuwa
amefuatana na mkewe, mama Janet Magufuli. Msafara wa Magufuli kuelekea
ofisi za CCM mkoani hapa uliondoka uwanja wa ndege Mwanza majira ya saa
8:30.
Akijitambulisha mbele ya maelfu ya
wakazi wa mkoa wa Mwanza waliofurika nje ya ofisi ya CCM mkoani hapa,
Dk. Magufuli aliwapongeza wananchi kwa mapokezi yao makubwa, huku
akiwataka Watanzania wote kuendelea kulinda umoja wao kwa nguvu zao
zote.
“Ninawashukuru
sana kwa mapokezi yenu makubwa…lakini pia ninawaomba muulinde umoja
wetu na tuendelee kushirikiana bila kujali itikadi za vyama wala rangi
zetu,”Dk. Magufuli.
Aliahidi kuisimamia kwa kikamilifu Ilani ya CCM. Alisema atahakikisha wafanyabiashara ndogo ndogo hawanyanyaswi.
Awali akimkaribisha, Dk. Magufuli, Nnauye
alisema CCM hakitasita kuwashughulikia wanachama wake ambao hulalamika
kwamba mchakato wa kuwapata mgombea urais kupitia chama hicho ulikiuka
taratibu.
“Ninapenda
kuwaambia kuwa mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama uliisha
salama na tulimaliza salama ingawa kuna baadhi ya watu wanalalamika
lalamika,” alisema.
Alisema wanaCCM hao watashughulikiwa na chama iwapo wataendelea na malalamiko hayo ambayo alisema hayana ukweli wowote.
“Wakiendelea tutawajibu, hasa wazee wetu.” alisema huku akishangiliwa.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk. Magufuli
kufika Mwanza tangu achaguliwe na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho
kuwania nafasi ya urais kupitia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25, mwaka huu.
NIPASHE
Abiria zaidi ya 100 wanaokwenda mikoa ya
Tabora na Kigoma wanaotumia usafiri wa treni wamekwama jijini Dar es
Salaam kwa siku mbili baada ya Kampuni ya Reli nchini (TRL) kusitisha safari bila taarifa.
Abiria hao wengi wao wanawake na watoto,
wamesema wanakabiliwa na hali mbaya ya kukosa chakula na huduma ya choo
na kuhatarisha maisha yao.
Laurent Mayee mkazi wa
Kigoma, alisema treni hiyo ilitakiwa kuanza safari juzi saa 11: 00 jioni
lakini hadi jana saa 8 mchana hawajaondoka na hakuna kiongozi
aliyejitokeza kutoa ufafanuzi.
Alisema yeye na ndugu yake ambaye ni
mgonjwa walilipia Sh. 55,400 kila mmoja kwa behewa la daraja la pili,
lakini tangu juzi asubuhi walipofika kituoni hapo wamejikuta wanasota
kusubiri usafiri huo bila kuwa na uhakika wa lini wataondoka.
Mayee alisema uongozi wa TRL wamekuwa wakibadilisha ratiba kila wakati kupitia ubao wa matangazo.
Alisema ratiba ya kwanza iliyobadilishwa
ilionyesha treni hiyo ingeanza safari saa 4:00 usiku, lakini ulipofika
muda huo ilibandikwa ratiba nyingine ikionyesha safari hiyo imeahirishwa
hadi jana saa 4:00 asubuhi.
Hata hivyo ratiba hiyo ilipanguliwa na
kueleza safari ingeanza saa 11 jioni huku hakuna ufafanuzi wowote wa
sababu za kuahirishwa kwake.
“Tangu
tufike hapa jana (juzi) tumekuwa kama tupo gizani, hatujui lini treni
itaondoka kitu kibaya zaidi tupo watu wengi tukiwa hatuna chakula,
hatujui tutaishi vipi kwa siku zote tukiwa hapa,” Mayee.
Abiria mwingine Hamisa Adamu anayesafiri
kwenda Kigoma, alieleza kwamba shida kubwa wanayokabiliana nayo ni
kukosa sehemu ya kulala na vyoo vya kujisaidia hasa kwa akina mama na
watoto ambao hawana uwezo wa kulipia huduma hiyo.
Hamisa alisema hakuna anayepingana na
kuwapo kwa tatizo, lakini ingetumika busara kwa viongozi kuongea na
abiria hao kwa kuwaeleza tatizo pamoja na kusaidia mahitaji mbalimbali
ya muhimu.
“Wewe
fikiria mama atapata wapi pesa ya kulipia huduma ya choo Shilingi 300
ya kila anapohitaji yeye na mtoto wake, huku hajapata chakula wala maji
tunaomba serikali kuingilia kati jambo hili haraka,” John Daniel.
Hata hivyo alipotafutwa Ofisa Habari wa kampuni hiyo Midladjy Maez kwa kutumia simu yake ya mkononi hakuweza kupatikana baada ya kuita bila kupokelewa.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba,
alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alisema hawezi kueleza chochote kwa
sababu yupo katika msafara wa mgombea urais kupitia CCM, Dk. John
Magufuli.
NIPASHE
Matatizo na manyanyaso yanayolalamikiwa
na Watanzania yanadaiwa kutokana na mfumo mbovu wa serikali iliyopo
madarakani inayotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kushindwa
kutetea maslahi ya wananchi wanyonge.
Tundu Lissu, aliwataka
Watanzania kutomchagua mgombea aliyepitishwa na CCM kugombea urais Jonh
Magufuli, maana hatakuwa na utendaji tofauti na viongozi waliomtangulia.
“Matatizo
na changamoto zinazowakabili Watanzania zimetokana na mfumo mbaya wa
CCM sio mtu, kwa hiyo wananchi wasimchague Magufuli wakidhani atatenda
maajabu au mapya yatakayowafanya kuondokana na changamoto hizo,” Lissu.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete,
alisifiwa sana wakati anachaguliwa lakini ameshindwa kutetea maslahi ya
wananchi na badala yake umekuwapo mfumuko wa bei na kuongezeka kwa
michango inayowaongezea maumivu wananchi.
“Wizi
wa fedha za EPA, Richmond na Escrow, mbunge wenu (jimbo la Muleba
Kaskazini) Charles Mwijage na Magufuli mbona hawakuwa na mtazamo tofauti
na CCM ili muweze kuwaamini wapo tofauti na viongozi wengine wa chama
hicho,” alihoji.
Alisema ili kudhihirisha CCM wanafanya
maamuzi ya kuwaumiza wananchi makusudi, maamuzi yaliyofanyika bungeni ya
kuletwa na kupitishwa kwa miswada ya dharura haikuwa mara ya kwanza
maana miaka 18 iliyopita, serikali ya CCM ilileta muswada wa madini kwa
dharura na sasa matokeo yake yanaonekana ya kuibwa kwa madini ambayo
yangekuwa mkombozi kwa Watanzania.
Katika mkutano huo ambao pia ulitumika
kumpigia debe mgombea ubunge katika jimbo la Muleba Kaskazini kwa tiketi
ya Chadema, Ansbert Ngurumo, diwani wa kata ya Kamachumu, Danstan
Mutagahywa, alitangaza rasmi kuhama CCM na kuhamia Chadema.
NIPASHE
Wimbi la watoto kutoroka majumbani
limeibuka ambapo jumla ya wanafunzi wanne wameripotiwa kutoroka huku
mmoja wa watoto hao akimwachia baba yake mzazi ujumbe kuwa ameamua
kufanya hivyo baada ya kukerwa na kitendo cha walimu wake kumuadhibu
bila kosa.
Wazazi wa wanafunzi hao waliofika kwenye
ofisi za The Guardian zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam,
walieleza mazingira tofauti ya kutoweka kwa watoto wao akiwamo huyo
aliyeacha ujumbe kwa baba yake.
Katika tukio la kwanza, mwanafunzi wa
kidato cha tatu, Murtaza Petro (16) wa Shule ya Sekondari Mikwambe,
ametoweka nyumbani na kumwachia baba yake ujumbe unaosomeka:
“Baba
samahani mimi naondoka kwa sababu walimu wamenikasirisha wamenipiga mno
bila kithibitisho wakasema nimekaa chimbo wakati sio kweli,’ baada ya
maelezo hayo aliikunja na kuandika juu yake kuwa,
“Sio kwamba sipendi shule bali kitendo nilichofanyiwa.”
Baba mzazi wa mtoto huyo, Petro Murtaza, alisema mwanae alitoroka nyumbani Mei 16, mwaka huu na kwenda kusikojulikana.
Alisema siku moja nyuma Murtaza aliadhibiwa na walimu wake kwa kosa la kwenda kukata nywele kwenye eneo ambalo shule imezuia.
Petro amemuomba mtoto wake popote alipo
arudi nyumbani ili aendelee na masomo yake na kuomba yeyote atakayemuona
apige simu namba 0757 877588 au atoe taarifa kituo chochote cha polisi.
Katika tukio la pili, mwanafunzi wa
darasa la nne, George Afumba (11) katika shule ya Msingi Atlas, jijini
Dar es Salaam, naye ametoroka nyumbani mara baada ya kutumwa na mzazi
wake akachukue nyanya gengeni.
Mama mzazi wa mtoto huyo Agnes Afumba alisema kuwa mtoto wake alitoroka wiki iliyopita na kwenda kusikojulikana.
Alisema mtoto huyo amekuwa na tabia za kutoroka nyumbani mara kwa mara na alipokamatwa hudai alikuwa kwenye michezo.
Alisema mara ya mwisho kutoroka ilikuwa
ni mwezi wa Aprili ambaye alikaa mtaani kwa muda wa siku tatu na kukutwa
kwenye baa ya Mango Garden akiangalia televisheni.
HABARILEO
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani
Katavi imemhukumu raia wa Burundi, Michael Lubandaya (18) kifungo cha
miezi sita jela kwa kosa la kujiandikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura akiwa si raia wa Tanzania.
Raia huyo wa Burundi ambaye ni mkazi wa
mjini Nyanza nchini Burundi anadaiwa kuingia na kuishi bila kibali
ambapo alijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa jina
la Abdallah Yusuph.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari
alisema mhamiaji huyo haramu anadaiwa kujiandikisha katika daftari la
kudumu katika kituo kilichopo kijijini Kakese – Mbugani na kupatiwa
kitambulisho cha mpiga kura chenye namba t1000- 4111-756-1.
“Katika
uchunguzi wa awali mtuhumiwa alibainika kuwa ni mkazi wa Burundi na
alijiandikisha huku akitambua kuwa si halali kufanya hivyo…baada ya
upelelezi wa awali mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na kuhukumiwa miezi
sita,” alieleza Kidavashari.
Katika tukio lingine mkazi wa Chamazi,
Dar es Salaam, Shaban Musa (38) amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya
Mpanda mkoani Katavi kwa kosa la kuingia ndani ya Kituo cha Polisi
Mishamo na kuanza kupiga picha za mnato pasipo halali yoyote.
Kamanda Kidavashashri akisimulia mkasa
huo alisema tukio hilo lilitokea Juni 29, mwaka huu saa kumi jioni
katika kijiji cha Ifumbula wilayani Mpanda ambapo alikamatwa akiwa
ameingia ndani ya eneo la kituo cha Polisi Mishamo na kuanza kupiga
picha bila ruhusa.
“Ni kwamba, siku ya tukio mtuhumiwa
alifika eneo hilo la kituo cha Polisi Mishamo na kuanza kupiga picha za
mnato kwa kutumia kamera ya simu yake aina ya Huawei Model Y300 – 0100.
Hata hivyo mtuhumiwa hakuishia hapo
aliamua kuelekea eneo lingine lililopo jirani na kituo ambalo kwa sasa
linajengwa kituo kipya cha Polisi na kuendelea kupiga picha.
Wakati mtuhumiwa huyo akiendelea kupiga
picha ndipo alipobainika na kukamatwa,” alieleza Kwa mujibu wa
Kidavashari uchunguzi wa awali wa tukio hilo, mtuhumiwa alibainika
kupiga picha ambazo zilileta mashaka kwani miongoni mwa picha alizokutwa
nazo ni za viwanja muhimu vya michezo ambavyo kuna kuwa na mikusanyiko
mikubwa ya watu, ofisi za kampuni ya wakulima(CAMCOS).
Picha zingine alizokutwa nazo ni pamoja
na vibao vya kutambulisha maeneo mbalimbali ya Mishamo, picha za kituo
cha Polisi mishamo ambacho kinafanya kazi na kinaendelea kujengwa na pia
inadaiwa alipiga picha kituo cha afya Mishamo, kituo cha Umoja wa
Mataifa cha Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na makazi ya viongozi hao wa
UNHCR.
JAMBOLEO
Migogoro ya ardhi wanayokabiliana nayo
wakazi wa Kata ya Dodoma – Makulu, kwenye Manispaa ya Dodoma, imeelezwa
kuwa itatumika kama kigezo kitakachotumiwa na wakazi hao, kuchagua
viongozi katika ngazi za udiwani, ubunge na urais, unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Hayo yalielezwa na baadhi ya wakazi wa
Mitaa ya Kisasa, Medeli na Bwawani, wakiwa kwenye ofisi za CCM za Kata
ya Dodoma Makulu walipomsindikiza mtia nia ya kuwakilisha chama hicho
katika uchaguzi wa diwani wa kata hiyo, Lazaro Chihoma, aliporejesha
fomu.
“Wakazi wa mitaa karibu yote ya kata
hii, tumekubaliana Chifu wetu (Chihoma) awe kiongozi wa kisiasa wa kata
yetu, kwa sababu kwa muda mfupi ambao amekuwa mwenyekiti wa serikali ya
mtaa wa Bwawani, ametetea haki zetu dhidi ya waliotudhulumu ardhi,”
Mchungaji wa Kanisa la Mitume, Yohana Mabene, alieleza.
Naye George Michael, mkazi wa Mtaa wa
Medeli, alisema mtaa huo hauna mwenyekiti kufuatia wananchi kugoma
katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini, kutokana na
aliyekuwa mwenyekiti kwa zaidi ya miaka kumi, Stanley Chibwete, kudaiwa
kuwa mgombea pekee aliyetakiwa kupigiwa kura.
Naye Chiloma ambaye pia ni chifu wa watu
wa kabila la Kigogo, akizungumza mara baada ya kuwasilisha fomu za
kuwania udiwani wa kata hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na diwani wa
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema ameridhia ombi la
wananchi wa kata hiyo na aliahidi kuwatumikia bila kuwaangusha.
Alisema endapo atachaguliwa kuwa diwani
wa kata hiyo, ataendelea kutumia njia ya mazungumzo na maafikiano, kati
yake kwa niaba ya wananchi anaowaongoza pamoja na mamlaka zinazohusika
na usimamizi wa matumizi ya ardhi, kuhakikisha kila mwananchi anapata
haki yake anayostahili.
No comments:
Post a Comment