Wednesday, 8 July 2015

Rais JK kuvunja Bunge, Tido Mhando na Wema Sepetu kuwa Mawaziri!? Wageni Dodoma je?>>>Stori Kubwa (Audio)

LAYIII
PB Clouds
Ni Jumatano nyingine tena na inawezekana uchambuzi wa magazeti leo kupitia @CloudsFM ulikupita, hiki ndio nilichokipata kwenye Uchambuzi wa stori kubwa za Magazetini.
Rais JK anatarajia kulihutubia na kulivunja Bunge kesho July 9 Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema baadhi ya wageni wanaoingia jijini humo watalazimika kulala nje ya Dodoma mpaka shughuli za Kiserikali zitakapoisha… CHADEMA wanafanya Mkutano kujadili mambo mengi ikiwemo kuangalia mchakato wa BVR.
Kuna stori pia kuhusu watu milioni 11  kuandikishwa kwenye daftari la wapigakura kwa kutumia mfumo wa BVR.
Mgombea Urais wa CCM, Maliki Malupu ametangaza Baraza la Mawaziri litakalokuwa na Mawaziri 18, Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kungozwa na Tido Mhando na Naibu Waziri kuwa Wema Abraham Sepetu.
Mbunge Joshua Nassari amenusurika ajali ya helikopta jana, yeye pamoja na wengine waliokuwepo kwenye ajali hiyo wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Uchambuzi wa stori zote uko kwenye hii sauti hapa niliyorekodi #PowerBreakfast.


No comments:

Post a Comment

advertise here