Tuesday, 28 July 2015

Lowassa kathibitisha kujiunga na UKAWA

LAYIII

LOWASA BREK
Ikiwa ni siku chache tangu Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kuenguliwa jina lake katika mbio za kuwania Urais na kamati ya maadili CCM, kumekuwepo na sintofahamu juu ya hatma ya mwanasiasa huyo.
Leo Lowassa kazungumza Bahari Beach, Dar es salaam pamoja na viongozi mbalimbali wa UKAWA walikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia hatma yake kuelekea Ikulu pamoja na upungufu uliojitokeza wakati wa uchaguzi wa kumpata mgombea Urais wa CCM.

Amesema baada ya kutafakari kwa kina na kujiridhisha ameamua kujiondoa CCM na kuitikia wito wa UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Amesema pia safari yake haitafanikiwa iwapo hawatajitokeza watu wengi kupiga kura, na anaiomba Tume ya uchaguzi NEC kuongeza muda wa kujiandikisha ili watu wote waweze kujiandikisha kama ilivyofanya katika Mikoa mbalimbali.
Pia amesema alinyimwa haki yake na CCM  kama Mtanzania kujieleza na kujitetea, hivyo atakua mnafiki akisema ana imani na chama hicho.

No comments:

Post a Comment

advertise here