LAYIII
DU! Kazi kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya
MAYASA MARIWATA
DU! Kazi kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya kukatwa jina kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliyekuwa mmoja wa watia nia ya kugombea urais, Amani lina mkanda kamili.
DU! Kazi kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya
MAYASA MARIWATA
DU! Kazi kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya kukatwa jina kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliyekuwa mmoja wa watia nia ya kugombea urais, Amani lina mkanda kamili.
Wema Sepetu alipokuwaakikabidhiwa fomu za kuwania ubunge viti maalum mkoa wa Singida leo mwishoni mwa wiki iliyopita.
DU! Kazi
kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari
zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya kukatwa jina kama
ilivyotokea kwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliyekuwa mmoja
wa watia nia ya kugombea urais, Amani lina mkanda kamili.
Aliyekuwa Mbunge wa Monduli na mmoja wa watia nia ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM walioenguliwa, Edward Ngoyai Lowassa.
ALIVYOENGULIWA LOWASSA
Lowassa alikuwa miongoni mwa makada 33
kati ya 38 walioenguliwa na Kamati ya Maadili ambayo ilipitisha majina
matano pekee katika kikao cha Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye
Mkutano Mkuu kupitisha Mbunge wa Chato, Dk. John Pombe Magufuli kuwa
mgombea urais kwa Tiketi ya CCM.
Wema Sepetu baada ya kuchukua fomu.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo kilicho karibu na staa huyo
kimepenyeza ‘ubuyu’ kuwa, Wema ambaye anashikilia Taji la Miss Tanzania
2006/07, ameingiwa na hofu hiyo baada ya kuona Lowassa ambaye ana sifa
ya kukubalika kama alivyo yeye ameenguliwa na kikao cha Kamati ya
Maadili ya CCM.
“Bibie (Wema) anajiamini, anakubalika
kweli lakini kitendo cha Lowassa ambaye alikuwa anaonekana kukubalika
kimemtia hofu na kuona kumbe kukubalika pekee si silaha ya ‘kuwini’
kupitishwa na chama,” kilisema chanzo hicho.
CHANZO CHAZIDI KUTIRIRIKA
Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi
kwa kudai hofu hiyo iliongezeka kwa Madam hususan baada ya kusambaa kwa
kuwepo kwa watu wasiompenda kupandikiza chuki kwamba baadhi ya skendo
zilizomgusa zinaweza kumpotezea sifa ya jina lake kupitishwa na
Halmashauri Kuu ya chama chake.
“Si unajua tena Madam kwenye maisha yake
ya sanaa amepitia skendo za hapa na pale, hiyo inaweza kuchangia kumtia
hofu maana wabaya wake wanaweza kuitumia kama silaha hivyo amekuwa
akitoa chozi na kumuomba Mungu amfanikishe,” kilisema chanzo hicho.
SKENDO INACHANGIA KUMPOTEZEA SIFA?
Duru mbalimbali za habari zinaonesha
kwamba kitu kikubwa kinachoangaliwa kwa kiongozi ni suala la
uwajibikiaji na si tabia binafsi au skendo.
Wapo viongozi ambao walikuwa na skendo
lakini wameweza kupitishwa na wananchi wao na kuwatumikia vizuri kuliko
hata wale walionekana wasafi.
“Si kweli kwamba skendo ndiyo kigezo
kikuu cha kumpitisha mgombea, mbona watu kama akina Mike Sonko (alikuwa
Mbunge wa Kenya), marehemu Amina Chifupa (alikuwa Mbunge Viti Maalum,
Vladimir Vladimirovic Putin (rais wa urusi) na wengine wengi, walikuwa
au walipata skendo lakini walifanya vizuri katika uongozi wao,” alisema
mwanaharakati mkubwa wa siasa nchini aliyeomba hifadhi ya jina.
NAPE ANENA
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kumuengua mgombea yeyote
kutokana na skendo au chuki zinazoezwa na baadhi ya wanachama wa chama
hicho, alisema si kweli bali wao wanafUata taratibu na kanuni
walizojiwekea na si vinginevyo.
“Sisi tuna kanuni na taratibu za chama,
hiyo ndiyo misingi yetu. Hatumuengui mtu kwa chuki binafsi wala kitu
kingine chochote zaidi ya kufuata kanuni zetu,” alisema Nape.
WEMA ANASEMAJE?
Akizungumza na mwanahabari wetu hivi
karibuni, Wema alikiri kupata hofu hiyo kwa muda lakini ameshajiamini
kutokana na kumuomba Mungu ambaye amekuwa akimtanguliza katika kila
jambo analolifanya.
“Kusema kweli mtu unapotaka kufanya
jambo unapaswa kujiamini, hata mimi mwanzo nilikuwa nimejipa matumaini
ya hali ya juu kwamba Lowassa atapita, lakini bahati mbaya akakatwa,
naamini Mungu yupo, mimi naswali usiku na mchana, Mungu atanisimamia
katika hili,” alisema Wema.
No comments:
Post a Comment