Tuesday, 26 May 2015

BEYONCE NA JAY Z NI MAHABA NIUWE TU KAMA WAMEANZA JANA VILE

NA LAYII
Rapa Jay Z na mkewe Beyonce wakijiachia kwenye viunga vya jiji la Florence nchini Italia.
Florence, Italia
PENZI ni kikohozi kulificha huwezi! Ndivyo ambavyo wanaonyesha wapenzi wawili maarufu duniani, rapa Jay Z na mwimbaji Beyonce ambao hivi sasa wapo nchini Italia wakila raha na
unaambiwa wamekuwa wakigandana na kuonyeshana mahaba hadharani utadhani walianza mapenzi yao jana kwa jinsi walivyoshibana.
Jay Z, 45, na Beyonce, 33, ambao kwa miezi kadhaa iliyopita walidaiwa wapo katika mgogoro wa ndoa, wameonyesha ndiyo kama mapenzi yao yameanza upya wakiwa wanakula bata katika Jiji la Florence.
Wawili hao ambao ni miongoni mwa wapenzi matajiri zaidi duniani, walionekana wakikatiza sehemu mbalimbali jijini humo huku wakionekana kuwa na nyuso za furaha.

No comments:

Post a Comment

advertise here