NA SWAXBZ LAYIIIIII
Nakupeleka
moja kwa moja kwenye jiji la Barcelona Spain, ni jiji ambalo mpaka
mwaka 2011 lilikua na watu zaidi ya milioni moja na laki sita ndani yake
na sasa wanasema kuna zaidi ya watu milioni 5 ambapo ni jiji la pili
kwa ukubwa kwenye nchi ya Hispania.
Unaambiwa usafiri huu wa Tram ulianza kufanya kazi kwenye mji wa Barcelona toka mwaka 1872 lakini barabara zilizokua
zikitumika na Tram za zamani zilifungwa ilipofika mwaka 1971 na nafasi yake ikachukuliwa na Mabasi pamoja na Treni za chini ya ardhi.
Kwenye hii picha ya juu na ya chini ni muonekano wa Tram za mwanzoni kabisa wakati Barcelona imeanza kutumia aina hii ya usafiri.
Baada ya mapito yote hayo sasa hivi mji wa Barcelona unatumia Tram za kisasa zinazopita kwenye njia yake ya reli kama kawaida na wamezitengenezea sehemu yake iliyo na mvuto zaidi kama unavyoona kwenye picha hapa chini na barabara hiyo usafiri mwingine wowote hauruhusiwi kupita.
Usafiri mwingine unaotumika sana Barcelona ni usafiri wa Treni za chini kwa chini, yani zinapita chini ya ardhi na kusafirisha watu kwenda sehemu mbalimbali ndani ya mji, ni usafiri maarufu kwa jina la Metro.
Mfumo wa nauli kwenye Treni hizi za chini maarufu kama Metro unatumia kadi kama za ATM ambazo unaweza kulipia safari nyingi na ukifika kwenye mlango wa kuingilia kama huu hapa chini unaipitisha ile kazi kisha mlango unakuruhusu kupita kuingia kwenye kituo na kupanda Treni ya safari yako.
Haya yote niliyapata wakati nikiwa Spain na mwenyeji wangu alikua ni Mtanzania anaitwa Mganga Yahya na mke wake ambaeo wameishi Spain kwa miaka zaidi ya 15.
Hapa chini nimekuwekea video inayoonyesha jinsi ya kununua Ticket, na usafiri wenyewe ulivyo.
Kumbuka hii ni chini ya ardhi, Metro huwa zinatumiwa na watu wengi sababu hakuna foleni na sasa usalama upo japo kuna wale Wanawake wa Romania wanaotajwa sana kuibia watu mifukoni ndani ya hizi Treni, ukiachia hiyo huu ni usafiri salama wa kuutumia na hamna wezi wa kukaba hata iwe usiku wa saa ngapi.

No comments:
Post a Comment