Friday 24 March 2017

RAIS JOHN MAGUFULI: NIKISEMA UKWELI, WATANZANIA WENYE UCHUNGU MTALIA!!!




Rais wetu kipenzi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, jana alifanya yale ambayo huwa anayapatia kweli kweli!! 

Kwa kutumia umahiri mkubwa kabisa, bila shaka aki-apply mbinu za kijeshi alizowahi kujifunza JKT, Mheshimiwa Magufuli aliingia bandarini kwa kushitukiza hali iliyowafanya watu wa pale wapigwe
butwaa huku wengine mioyo yao ikipiga mkamba kwa sababu hawakutarajia kutokea Mheshimiwa huyo!!!

Mbinu hizi za kijeshi, na bila shaka zikichanganyika na mbinu za kijasusi; zilimwezesha Mheshimiwa Rais wetu aweze kukamata makontena kadhaa yaliyojaa dhahabu!!! 

Huku akionekana kujawa na uchungu kwa nchi yake, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alisema:
Kwa taarifa nilizonazo, nikizisema hapa mnaweza mkalia! Dhahabu iliyopo humu ndani! Kwa Mtanzania yeyote anayeipenda Tanzania... atalia! Kwa mali zilizomo humu...!

No comments:

Post a Comment

advertise here