Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa msanii Nay wa Mitego usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro.
Kamanda Ulrich Matei ametoa sababu kubwa ya kukamatwa kwa msanii huyo ni kutokana na kutoa wimbo unaofahamika kwa jina la 'Wapo' ambao anadai unaikashfu Serikali iliyopo maradakani.
Kamanda Matei amesema shauri la Nay wa Mitego lipo jijini Dar es Salaam hivyo msanii huyo atasafirishwa na kupelekwa Dar es Salaam kuhojiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa.
"Ni kweli huyu Bwana anashikiliwa Morogoro na shauri lake sio la Morogoro, tulipata tu maelekezo kwamba tumtafute",amesema kamanda
No comments:
Post a Comment