Saturday, 10 December 2016

WASANII WACHACHE WALIOCHEZEA BAHATI KTK TASNIA YA MUZIKI

Hapana shaka hata kidogo mziki wa Bongefleva umepanda chati kwa kasi sana kimataifa hasa barani afrika na wanamuziki wake wamekuwa na ushawishi mkubwa katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi..
Mpaka mziki huu umefanikiwa kufika hapo imekuwa ni safari iliyojaa milima na mabonde! Kuna ambao mziki umewapatia ajira na wametoka kimaisha na wapo ambao walichezea shilingi kwenye shimo la choo..


BIGGEST LOSERS

5. RAY C

Rehema chalamila (maarufu Ray C) alitikisa vya kutosha mwanzoni mwa miaka ya 2000 (2003 - 2007). Alijijengea mpaka image na heshima ya kuonekana ni moja ya malkia wa kiwanda cha mziki Tanzania akiwa sambamba na kina lady jaydee.! Dalili mbaya zilianza baada ya kuwa na ukaribu na Nako 2 Nako na hasa kiongozi wa kundi la N2N, lord eyez! Baadae wakanzisha mahusiano na muda si muda akajitumbukiza kutumia madawa ya kulevya and the rest is history.. Amepotea kwenye game na hakuna tumaini kama atarudi!!


4. 20 PERCENT

Mpaka sasa ndiye msanii namba mbili kwa kuzoa tuzo nyingi kwa usiku mmoja baada ya kuzoa tuzo 5 za KTMA mwaka 2013! Kuna kipindi ilikuwa kila nyimbo atakayoitoa muda mchache tu inageuka 'nyimbo ya taifa' inaimbwa mpaka na mtoto Mdogo anayejifunza kuongea.. Kizuri zaidi nyimbo zake zilikuwa na ujumbe kiasi hata leo hii ukisikiliza bado unaburudika.. Kilichotokea kwake mpaka kushuka na hatimaye kupotea kabisa kwenye game anakijua yeye pamoja na producer wake Man water.. Sijui ni mibangi au walikorofishana tu lakini kiwanda cha mziki tumepoteza kichwa hapa..


3. MARLAW

Moja kati ya mazingaombwe ya Bongofleva ambayo bado siyaelewi mpaka leo moja wapo ni hii!! Inawezekana vipi mtu mwenye kipaji, mashabiki, na influence kama Marlawa anapotea moja kwa moja??? Tatizo ni nini? Familia? Mbona kuna wasanii wengi tu wanafamilia na wanafanya vizuri?? Au kampeni za siasa 2010 ndio zilimponza? Lakini mbona ni wengi walishiriki zile kampeni lakini mpaka leo bado wanafanya vizuri?? Alafu kinachoshangaza mpaka leo jamaa ukimsikiliza anaimba unaona kabisa bado anajua?? Sijui ni nini kimemkuta.. Lakini kuna kipindi alipokuwa kwenye ubora wake aliiteka Bongofleva yote!


2. CHID BENZI

Hakuna cha Joh Makini, hakuna cha stamina, hakuna Niki mbishi wala young dee au sijui young nani.. Huyu ndio alikuwa mfalme wa Bongo Hip Hop na alipokuwa katika ubora wake aliiweka Bongofleva nzima kwenye kiganja cha mkono wake.. Walaaniwe wauza unga wote!


1. MR. NICE

Alikuwa ndiye diamond wetu, Alikiba wetu, Navy kenzo wetu.. Mpaka leo bado sijaelewa kinagaubaga hasa nini kilitokea, alibahatisha? Alifanyiwa figusu? Watu walichoka nyimbo za watoto? Alijisahau au pace ya ukuaji wa mziki ilimshinda akajikuta anakaa benchi bila kupenda??

No comments:

Post a Comment

advertise here