Gift Stanford ‘Gigy Money’.
Ma-video queen wasumbufu Bongo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ na Gift
Stanford ‘Gigy Money’ wapo kwenye vita baridi (vita ya maneno) kufuatia
Gigy kumchamba mwenzake kutokana na yale madai ya kukamatwa na ‘unga’ jijini Arusha.
Lulu Euggen ‘Amber Lulu’.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa baada ya habari kuzagaa
kuwa Amber Lulu amekamatwa na polisi Arusha akiwa na unga, Gigy amekuwa
akimsema mwenzake huyo vibaya, mazingira yaliyosababisha wawili hao
waanze kuraruana kwa maneno.Akizungumza hivi karibuni, Amber Lulu alisema: “Nawashangaa hao wanaonisema vibaya kufuatia hizo tetesi, hasa Gigy ila siwezi kujibishana naye kwani siyo levo yangu.”
Gigy naye akafunguka: “Ni kweli nilimsema kuwa kama kweli kakamatwa na unga atakuwa katuaibisha sana. Huo ndiyo ukweli sasa akitokwa na povu atokwe tu.”
No comments:
Post a Comment