Waziri wa maswala ya ndani wa ufaransa , Bernard Cazeneuve, ametoa
ushauri kwa wakuu wa miji mbalimbali wenyeji wa kinyanganyiro cha soka
barani ulaya Euro2016, kupiga marufuku matumizi ya pombe katika maeneo
tete siku ya na hata kabla ya siku ya mechi kufanyika.
Hii ni kutokana na matukio ya wafuasi wa timu kadhaa kushambuliana
katika visa vilivyochochewa na ulevi huko mjini Marseille katika kipindi
cha siku 3 zilizopita.
Shirikisho la kandanda barani ulaya ,
UEFA, limeonya kuzichukulia hatua ya hata kuwafurusha kutoka mashindano
hayo timu za Uingereza na Urusi iwapo mashabiki wao watajihusisha tena
na matukio ya ghasia kama ilivyotokea wakati wa mechi yao katika mji wa
Marseille .
Ulevi unatajwa kuwa ni moja ya vyanzo vya vurugu hizo ambapo baadhi
ya mashabiki wana kwenda katika viwanja vya michezo wakiwa wamelewa
chopi.
Serikali ya Uingereza tayari imeahidi kutuma idadi kubwa ya
maaskari wa kupambana na fujo kabla ya mechi ijayo inayohusisha timu ya
Uingereza siku ya Alhamisi.
Bwana Cazeneuve amenukuliwa akisema
''Tutafanya kila tuwezalo kuzuia ghasia na machafuko zaidi ikiwemo
kuzuia uuzaji wa pombe unywaji wa pombe na hata usafirishaji wa pombe
kuelekea maneo wenyeji wa kombe la Euro''
''Tutaweka marufuku ya pombe katika maeneo yote ya umma'' Vilevile baa na migahawa inayouza tembo italazimika kubadilisha
mikebe na chupa wanayouzia pombe ilikuzuia madhara yanayotokana na
walevi kutumia vyombo hivyo kama makombora haswa dhidi ya polisi''
alisema bwana Cazeneuve.
No comments:
Post a Comment