layiiii
Huku dunia ikiwa bado haijaweza kumaliza hali ya mshangao ulioibuka kufuatia taarifa za kujiuzulu kwa rais wa FIFA, Sepp Blatter.. taarifa kadhaa nyumbani kwa Rais huyo nchini Uswisi zinadai kuwa huenda akarejea tena madarakani.
Gazeti moja la kila siku nchini Uswisi la Schweiz am Sonntag
limechapisha habari isemayo kuwa huenda rais huyo akarudi madarakani
kufuatia kuombwa kufanya hivyo na vyama kadhaa vya soka katika mabara ya
Afrika na Asia.
Headline ya Schweiz am Sonntag imeandikwa hivi >>> “Sepp Blatter soll Präsident der Fifa bleiben (Sepp Blatter to remain president of Fifa)“>>>
Chanzo kingine kilicho karibu na Blatter
kimesema kuwa rais huyo amefikiria kurejea madarakani japo bado
hajaweka wazi azma hiyo na kwa jinsi mambo yanavyokwenda anaweza kurudi.
Blatter alichaguliwa kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa FIFA akimshinda makamu wake wa Rais, Prince Ali Bin Al Hussein kabla ya kuamua kujiuzulu siku nne baada ya uchaguzi huo kufuatia mfululizo wa kashfa za rushwa ulioikumba FIFA.
Hadi sasa viongozi kadhaa wa
FIFA wamekuwa wakifanyiwa uchunguzi kuhusiana na kashfa hii ambayo
imesababisha mgogoro mkubwa na hali ya sintofahamu kwenye shirikisho
hili la Kimataifa la mchezo wa soka
No comments:
Post a Comment