Baraza la Sanaa Taifa ‘BATASA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili kutokana na wimbo huyo.
Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.
Baraza hilo limedai kuwa msanii kama ilivyo kwa raia yeyote anaweza kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kama kazi yake ikibainika kuwa na kosa la jinai.
“Tulifanya mazungumzo na wenzetu jeshi la polisi waliokua wanamhoji msanii Nay wa Mitego na kuchunguza jinai katika wimbo wake wa Wapo,” Basata walitweet.
Aliongeza, “Baada ya ushauri kutoka kwa Waziri Mwakyembe na baadaye taarifa ya jeshi la polisi na mazungumzo na msanii Nay kituo cha kati cha polisi.Tunaruhusu wimbo wa ‘Wapo’ wa msanii Nay kuchezwa katika vyombo vya habari. Kama taarifa yetu ilivyoeleza, ulisitishwa kupisha taratibu za kipolisi,”
Rapa huyo aliachiwa jana jioni na jeshi la polisi kwa kauli ya Rais Magufuli baada ya kushikiliwa kwa siku mbili.
No comments:
Post a Comment