Sunday, 19 February 2017

BARNABA KAONGEA KUWA HANA MATATIZO NA MKEWE

BONYEZA PICHA HAPA JIUNGE NAMI YOUTUBE HABARI KWA NJIA YA VIDEO USIACHE KULIKE SHARE NA SUBSCRIBE

Mwimbaji wa bongofleva Barnaba Boy yupo kwenye vichwa vya habari za burudani kwa zaidi ya siku 5 sasa hivi baada ya habari zinazodaiwa kwamba ameachana na Mama mtoto wake.

Barnaba amehojiwa na The weekend chat show na kusema hayo ni maneno ya watu tu ila yeye hajagombana na mama watoto wake Mama Steven japo kila mtu ana matatizo.


“Mimi na wife wangu hatuna matatizo, maneno hayo yanayoendelea uko nje achana nayo, Mimi sijawai kugombana na mama watoto wangu wala mama watoto hajawai kuondoka nyumbani na the Good Thing is mimi na familia yangu tupo karibu na Steven anaenda shule kama kawaida“

“Chukua hili neno kubwa sana MIMI NA MAMA WATOTO WANGU HATUNA MATATIZO, kila mtu anamatatizo lakini mimi sidhani kama matatizo yangu naweza kuyaleta hadharani  ila natanguliza samahani kwa watu wangu kwa sababu mimi sipendi kelele mbaya”

“kwenye muziki wangu, Mungu anisamehe huu mwezi umekuwa kama unaniandama kwa vitu vingi sana ila Namuamini Yesu na namwamini Mungu kilicho kibaya kilicho kizuri namuachia Mungu“

No comments:

Post a Comment

advertise here