Saturday 7 May 2016

KWA MARA YA KWANZA JIJI LA LONDON LAPATA MEYA WA KIISLAMU

Like page yetu hapa FACEBOOK

j
Meya wa Lndon Sadiq Khan  
Jiji la London limemchagua Meya wa kwanza Muislamu, Sadiq Khan, aliyekuwa wakati mmoja Waziri katika chama cha upinzani cha Laba.
Bwana Khan ni mwana wa dereva wa zamani wa bas jijini London aliyezaliwa Pakistan. Alipata kura milioni moja na mia tatu elfu.

Hicho ni kiwango kikubwa sana cha kura kuwahi kupigiwa Meya ye yote jijini London.
Sadiq Khan akishirikiana na wakaazi wa jiji la London 
Katika hotuba yake ya ushindi, Bwana Khan aliahidi kuongoza kwa niaba ya wakaazi wote wa London.
Wasimamizi wa kampeni ya mpinzani wake katika uchaguzi huo Zac Goldsmith, ambaye ni tajiri mkubwa walishutumiwa kwa kudai kuwa Bwana Khan ana uhusiano na Waislamu wenye itikadi kali.
Bwana Khan alisema kuwa wakaazi wa London wamepiga kura ya umoja na kuponza mgawanyiko.


Ushindi huo ni wa kumtia moyo kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn.
Chama chake kilipata ushindi dhaifu katika maeneo mengine ya nchi katika uchaguzi huo.



No comments:

Post a Comment

advertise here