Saturday 10 October 2015

KWELI WATU WANATOKA MBALI ONA WANASOKA HAWA KABLA YA KUPATA MAFANIKIO

LAYIII
Katika maisha kuna mambo mengi ya kupitia hadi kufikia mafanikio mara nyingi au kwa asilimia kubwa wengi waliofanikiwa katika maisha walihangaika kufikia kilele hicho cha mafanikio kiasi hata cha kufikia kuwa mfano mzuri kwa vijana wanaohangaika kusaka mafanikio katika soka. October 11 naomba nikusogezee kazi za kwanza za mastaa hawa wa soka.

1- Angel Di Maria ni mchezaji ambaye wengi tumeanza kumfahamu vizuri kupitia vilabu vya Real Madrid na Manchester United kabla ya dirisha la usajili la mwezi August alipoamua kujiunga na PSG ya Ufaransa, unaweza ukafikiria ametokea katika familia ya kitajiri ila Di Maria amewahi kufanya kazi katika sehemu ya kuhifadhia makaa ya mawe akiwa yeye, wazazi wake pamoja na dada zake Vanesa na Evelyn lakini leo  hii ni staa na tajiri mkubwa kupitia soka.
di-mariaaa
2- Zlatan Ibrahimovic akiwa na umri wa miaka 15 alikaribia kuachana na soka na kutaka kutafuta maisha kwa njia nyingine kabla ya meneja wake kumshawishi asifanye maamuzi hayo, Zlatan alikuwa akiacha kucheza soka na kwenda kufanya kazi katika vivuko vya pwani ili apate fedha ya kujikimu. Lakini sasa anatajwa kuwa moja kati ya wachezaji bora duniani.
Zlatan-Ibrahimovic-PSG
Zlatan Ibrahimovic
3- Alex Sanchez  mshambuliaji wa kimataifa wa Chile anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza ambaye amewahi kutamba katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania. Sanchez kabla ya kuanza kupata mafanikio katika soka aliwahi kufanya kazi ya kuosha magari kabla ya soka kuwa mkombozi wa maisha yake.
Alexis_sanchez_3153909b
Sanchez
4- Carlos Bacca ni mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia na klabu ya AC Milan ya Italia ambaye kabla ya kuanza kupata mafanikio alikuwa mvuvi kwa kipindi kirefu kidogo na alikuwa msaidizi wa dereva, mpira ulikuwa kama sehemu ya kujifurahisha, historia yake inaonyesha katokea mtaani na kuanza kucheza soka katika timu ya Atlético Junior.
2C865B7900000578-0-image-a-182_1442699678244
Carlos Bacca
CGCf583WoAAC6nI
Carlos Bacca enzi za uvuvi
5- Frank Ribery ni winga wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, amewahi kupitia misukosuko mingi katika maisha yake, akiwa na umri wa miaka miwili Ribery alipata ajali ya gari pamoja na familia yake kitu ambacho kimemfanya abaki na makovu usoni hadi leo hii, Ribery aliwahi kufanya shughuli za ujenzi pamoja na baba yake, yote hiyo ilikuwa ni katika harakati za kutafuta maisha.
franck-ribery-in-neuem-look-auf-dem-weg-zu-alter-staerke-
Frank Ribery

No comments:

Post a Comment

advertise here