Maajabu ya kuvutia.. yani zimetengenezwa nyumba na Hotel kwa ubunifu wa nguvu mtu wangu.
Nyumba za vioo, nyumba za miti.. Ziko nyingi hapa mtu wangu, unaweza kuzicheki
zote.
Free Spirit Spheres, Canada. Utalii mwingine mzuri ndani ya nchi hiyo.
Boat Hotel. Hii Hotel vyumba vyake viko kama boti hivi, iko Visiwa vya Maldives, Asia.
Trojan Horse Hotel.
Kwa haraka haraka unaweza usijue hiki ni nini, lakini unaambiwa hii ni
Hotel, hapo ndani kuna vyumba vya kulala na kila kitu kinaenda poa
kabisa.
Ark Hotel, China.
Wachina na teknolojia zao mtu wangu, hii Hotel imetengenezwa kwenye
maji inaelea yani. Hapo unaweza kuona kwa juu inavyoonekana na kwa ndani
ya maji pia.
Mirror Tree House, Sweden.
Hapo panapoonekana kama mwanga mwekundu ni chumba cha Hotel yani,
kimejengwa kwa vioo vitupu. Utakuwa na amani kweli kulala hapo?
Castle Hotel, Austria. Yani ni kama unauangalia Mlima hivi, karibu sana Austria mtu wangu.
Unadhani hii ni karavati ya barabarani? Hapana.. Ni vyumba vya Das Park Hotel, iko Austria. Vyumba nd’o viko hivyo yani. Mambo ya Ulaya Ulaya.
Umeielewa hii? Ni Hotel inayoitwa Airplane, iko Costa Rica. Hapo vipi mtu wangu, umevutiwa na hii?
Bubble Hotel, unaweza kujionea hiii mtu wangu ukitembelea Ufaransa.
Moja ya story zilizosikika March 2015 ni malalamiko ya baadhi ya watu
kwamba hakuna usiri wowote ukiwa ndani ya chumba hicho cha Hotel.
Utajisikiaje
kuwa kwenye hiki chumba cha kioo? Aina hii ya kioo ni kama kile kioo
cha kujiangalizia.. mtu aliye nje haoni ndani. Hiki ni chumba cha Mirror Hotel, Berlin Ujerumani.
Hotel hii iko chini ya maji visiwa vya Fiji mtu wangu.
Magic Mountain Hotel, hii iko Panguipulli, Chile. Ukiiangalia kwa haraka ni kama Mlima uliozunguka na vichaka, hiyo ni Hotel mtu wangu.
Nitafurahi ukiniandikia wewe umeipenda ipi hapo mtu wangu?
No comments:
Post a Comment