Thursday 22 September 2016

NAVY KENZO NDANI YA MTVMAMA

Kundi la Navy Kenzo ambalo linaundwa na Aika na Nahreel limefanikiwa kuingia katika Mchakato (Nomination) wa kutafuta washindi wa MTV Mama Awards 2016 Kwenye kipengele cha Group Bora la Muziki Afrika,

Nimeanza na kuandika Hard Work Pays Kwasababu ni dhahiri kuwa hawa jamaa wamefanya kazi
hasa katika miaka ya karibuni katika kazi zao za muziki huu wa Bongo Flava Hapa Tanzania, Ukiangalia nyimbo zao za hivi karibuni kama Game na Kamatia chini ni nyimbo ambazo waliamua kuwekeza pesa hasa ili kufika kiwango cha kimataifa na kuweza kuwafanya wajulikane Afrika nzima
Hawa ni Mfano mzuri sana wakuigwa na wasanii wengine wa hapa Bongo , Katika tuzo hizo Kutoka Tanzania Wasanii walioweza kufanikiwa kuingia katika mchakato Navykenzo, Diamond na Ali Kiba...

Kazi imebaki kwetu mashabiki kuwapigia kura ili waweze kushinda Tuzo Hizo

No comments:

Post a Comment

advertise here